Jun 10, 2015

URAIS 2015 WASANII VIPANDE

MPASUKO! Zikiwa zimesalia takriban siku 31 kabla ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumpitisha mgombea mmoja wa urais atakayechuana na vyama vya upinzani, imebainika kuwa mastaa wa filamu na Bongo Fleva wamegawanyika vipande huku wakiwa kwenye msuguano mkali kufanikisha ushindi wa makada Bernard Membe na Edward Lowassa, Risasi Mchanganyiko linapa mchapo kamili.
Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe.WAJIPAMBANUA

Taarifa kutoka ndani ya tasnia hizo ambazo zina nguvu ya ushawishi katika jamii zimeeleza kuwa, Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kwa kiwango kikubwa amewakamata wasanii wengi wa Bongo Movies wanaomuunga mkono huku Lowassa (Waziri Mkuu wa zamani) akiwa amewadhibiti vilivyo mastaa wa Bongo Fleva.“Ni mpasuko wa aina yake, Membe ameonekana kuwakamata kisawasawa wasanii wa Bongo Movies na ndiyo maana hata juzi (Jumapili iliyopita), mastaa wengi wa filamu walikwenda Lindi kumuunga mkono alipokuwa anatangaza nia.
Membe akiwa na wasanii wa bongo movie.


WANACHOKIAMINI

“Mastaa kama Steve Nyerere (Steven Mengere, JB (Jacob Steven), Ray (Vincent Kigosi), Dude (Kulwa Kikumba, wanaoonekana katika picha ndogo ukurasa wa kwanza) Hashim Kambi, Ester Kiama (Ester wa Dude) Swebe (Adam Melele) na wengine kibao wameshatonywa kuwa CCM itampitisha Membe hivyo wanamuunga mkono kwa nguvu zote kuhakikisha wanapata sapoti pindi atakapopitishwa na chama chake kisha kuwa rais.


WENGINE HAWAJIPAMBANUI

“Timu ya wasanii wa filamu wanaomuunga mkono Membe ni kubwa sana sema wengine hawajajitokeza hadharani lakini wanapambana chini kwa chini kwani wana uhakikia kwamba piga ua, CCM itampitisha tu.
Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.


LOWASSA SASA

“Kwa upande wa Lowassa, amepata zaidi mastaa wa muziki. Nao wameamua kujipambanua kwa kuwa nao wametonywa kwamba rais ni Lowassa. Wanaamini hivyo, wanapambana kweli kuhakikisha anachukua mikoba ili aje awatimizie mahitaji yao.


“Utakumbuka wiki chache zilizopita alitangaza nia kule Arusha wasanii kibao wa muziki wakiongozwa na Diamond (Nasibu Abdul), Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki), Khadija Kopa na wengine wengi tu walienda kumuunga mkono. Kuna nyimbo 21 maalum za Lowassa zilizotungwa na wasanii mbalimbali na kusambazwa kama njugu kwa makundi tofauti ya watu wakiwemo waendesha bodaboda.
WAPO WA CHINI KWA CHINI

“Kama ilivyo kwa Membe, Lowassa naye ana timu kubwa sana katika Bongo Fleva ambayo inapambana chini kwa chini. Kuna wasanii kama R.O.M.A (Ibrahim Mussa), Juma Kassim (Nature), Recho (Winfrida Josephat) wote ni Team Lowassa. Yaani uchaguzi wa mwaka huu ni full mpasuko,” zilieleza taarifa hizo.MBIVU MBICHI, JULAI 12

Kwa mujibu wa ratiba ya chama cha mapinduzi CCM, mgombea wa urais atajulikana Julai 12, mwaka huu mara baada ya kikao cha Mkutano Mkuu kumalizika.

Jun 8, 2015

Mfanye Mpenzi Wako Unayempenda Achanganyikiwe Juu Yako Na Kukupenda Zaidi.

"Kwenye mahusiano ya kimapenzi ni vizuri uzito wa mahusiano uwe pande zote mbili, mapenzi huwa matamu zaidi iwapo umpendae naye anakupenda kwa kiwango umpendacho wewe, na si vinginevyo maana tofauti na hapo mapenzi huwa kama kero au mzigo na hisia hukupelekea kujiumiza moyo na kujiharibu kisaikolojia".
Wewe ni mtu mzuri na unampenda sana msichana wako, kiasi kwamba unamkubali sana mpaka unampa dunia yako kumuonyesha unavyomjari, ndani ya muda mrefu mliopo kwenye uhusiano umeshajitoa kwa mengi, kimuda na hata kifedha, unamchukua kutoka kazini kila siku ndani ya juma ili tu asije kuchosha miguu yake mizuri na laini.


Unamsaidia kwa kila jambo analohitaji na umeacha kutumia muda wako na marafiki zako ili kusudi uwe na muda mwingi zaidi wa kutumia naye, umemnunulia gauni la gharama na vingine vingi ili apendeze bila kuchoka huwa unabadilisha ratiba zako ili ziweze kuendana na za kwake ili muwe pamoja na kumuonyesha jinsi gani alivyo na nafasi kubwa ndani ya moyo wako, na unafanya yote haya bila ya kumtaka kitu chochote kutoka kwake.Na hata hivyo ni mara moja tu siku ule ulipokua unaumwa ambapo ulimuomba akupikie ugali na akakuchukulie mishikaki unayoipenda pale uswazi teki awei, ambapo alikataa kwa upole na kukwambia hajui kupika vizuri ugari na wewe ulikubali kwa roho safi maana hupendi kuwa kero kwake.
Sasa turudi kwenye uhalisia.

Rafiki sijui nikuambieje ili unielewe, kaka hapa unatiketi moja tu inayokwenda bila kurudi ambayo kupeleka kwenye nchi ya mvunjiko wa moyo ambapo wapo wapenzi wake wa zamani aliowaacha.
Ni muda wa kumuuliza, "Hivi ni kipi umenifanyia mimi hivi karibuni?".Kila ukiwa unamfanyia kitu kizuri nahisi labda unaona kama unajiongezea pointi nyingine za ziada, lakini kiukweli ni kwamba kama yeye hatojihusisha na kuchangia kwa kukufanyia wewe hayo mambo mazuri unayomfanyia yeye kwenye uhusiano wenu, jua kabisa nguvu zako zitakua hazina faida yeyote ile, ni kama maji mtaroni yanayopita tu, na hapa ndipo  tunapokwambia kwanini!.
Kikawaida tunaweza kuwapa ushauri wanaume wengi wanaokutana na haya wavunje uhusiano tu pale mwanamke anapomtumia mwanaume bila kurudisha upendo wowote ule anaofanyiwa, hapa simaanishi yale mambo yetu mengine ya kitandani.Lakini kama kweli umejiweka kwenye huu uhusiano kwa roho yote na unataka uhusiano uendelee kuwa wa muda mrefu lazima ufanye na yeye awekeze hisia zake na hata pesa zake kwenye huu uhusiano hata kama ni asilimia 50%.
Hapa haijarishi wewe ni tajiri kiasi gani, ni mzuri kiasi gani au ni mwanaume mwenye mahaba yote duniani kiasi gani, kama mwanamke hana kitu chochote alichowekeza kihisia, iwe ki muda au ki fedha lazima atakuacha iwapo mtu mwingine ambaye yuko zaidi ya wewe akitokea. Kama sheria  zinavyosema(kama msomaji utakua unazijua), "Mtu mpya na ambaye ni zaidi yako huwa yuko nyuma anakuja, anasubiri ukosee kidogo tu", na kama hata jiwekeza kwako likija dili ambalo ni zaidi ya wewe unalompa lazima ataondoshwa tu
Bado hujaniamini tu?

Kama ukiwekeza kiasi fulani cha muda na fedha kwenye mpango flani, iwe kununua nyumba au kuanzisha biashara, utakua unajua uchungu na uzito wa kitega uchumi chako tofauti na ukiwa umepewa bure.

Sheria hizi hizi ndizo zinazofanya kazi kwenye mapenzi, ni ubinadamu kuona uzito na uchungu kwenye kitu ambacho umekiwekeza, sasa nini swali kwako, "Ni nani anayechangia sa kwenye uhusiano wenu?, ni wewe au ni malaika wako mrembo?
Fikiria kwa umakini maana uhalisia wa jibu lako tayari limeshafanya kazi kubwa kuutengeneza uhusiano wako jinsi ulivyo sasa.Mwachie baadhi ya malipo afanye yeye...

Inabidi uwe kama vocha isiyorudishwa, fikiria kila saa msichana wako akienda kununua mahitaji yake, analipia kwa vocha na anapata muda wa maongezi, atafanya hivi kwa kipindi kirefu mpaka ndani ya muda atakuwa na muda wa maongezi ambao anaweza kuutumia kuongea kwa miaka mingi, sasa vipi kampuni nyingine ya vocha ikiingia na kumpa ofa nzuri zaidi?, kwa unavyofikiria anaweza kubadilisha kampuni?


Kama hata kuwa na muda wa maongezi mwingi na wewe, basi kuna nafasi kubwa atabadilisha kampuni bila kujiuliza na kwa upande mwingine kama atakua na muda wa maongezi mwingi wa miaka kumtosheleza maongezi yake kutokana na jinsi alivyowekeza, hawezi kubadilisha kampuni. Umeipata pointi yamgu, Rafiki?Kazi yako...

Ni kazi yako kumfanya msichana wako awekeze muda na hela kwenye kampuni yako ya vocha ili ikija kampuni nyingine isiweze kumchukua akili kwa ofa nzuri itakazokuja nazo.
Kwa kuwa sasa hivi nimeshakuelewesha umuhimu wa kumfanya msichana wako awekeze kwenye uhusiano, sasa utafanyaje ili aanze kuwekeza?Omba misaada: Kitu muhimu cha kuangalia sasa hivi ni misaada, kama akikupa msaada atajishauli amefanya hivyo kwa sababu unamvuto kwake na unastahili kufanyiwa hicho alichokifanya, acha sasa hivi akuhudumie vizuri, mwache sasa hivi akupikie, saa zingine mwombe aje akupitie kazini na mwache alipie baadhi ya vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wake.
Ukiishiwa vocha usione aibu kumtumia tafadhari niongezee salio mara moja moja.
Hii ni moja ya sababu hutakiwi kuweka mayai yote kwemye kapu moja, na ndio maana huwezi kumwacha mwanamke ambaye hakujali kwa sababu wanaume wengi wanakuwa wamewekeza muda mwingi na fedha kwa huyo mwanamke.Muda ni pesa: unaweza kumwongezea hamasa zake kwako kwa kumfanya atumie muda mwingi na wewe kwa kufanya vitu unavyovipenda na sio anavyovipenda, hii itamuonyesha uzito wako kwake.
Sio mbaya kumbeba mwanamke kama dhahabu, ila hakikisha ndani ya uhusiano kila mmoja anawekeza na sio uhusiano uwe unaegemea upande mmoja tu, kama kweli anahisia na wewe basi hisia zake zitamwendesha na yeye akujali wewe kama ambavyo zinakuendesha wewe.

May 31, 2015

BINTI AMUUA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA KUMLAZIMISHA KUFUA NGUO CHAFU!!

Si jambo la kawaida kusikia mtoto kamuua mama yake ama mama kamuua mtoto wake, japo kwa miaka ya sasa matukio kama hayo yameshamiri kwa kiasi kikubwa sehemu mbalimbali duniani.
Tukio la mtoto kumuua mama yake leo limechukua headlines huko Zimbabwe baada ya kutokea kutoelewana baina yao.


Kilichotokea ni kwamba binti wa miaka 17 amemuua mama yake kwa kumchoma moto baada kulazimishwa kufua nguo chafu, kitendo kilichomkasirisha na kufikia uamuzi huo.
Kabla ya kumuua mama yake kwa kumwagia mafuta kisha kumchoma moto, mama yake alimpiga kitendo kilichomuuzi binti huyo  na kufanya uamuzi huo mgumu.
Polisi wamemfungulia mtoto huyo mashtaka ya mauaji licha ya kupewa taarifa kuwa alikua akisumbuliwa na ugonjwa wa akili.

MSICHANA WA MIAKA 17, ABAKWA NA WANAUME 40

Katika moja ya makala gazeti la Sunday Times, Msichana mmoja jamii ya Yazidi, huko Syria ameweka wazi mateso aliyokuwa akipewa na kundi la wapiganaji wa kiislamu wa ISIS na kusema kwamba aliwahi kubakwa na wanaume wapatao 40 nakutolewa usichana wake.

Msichana huyo ambaye (jina limehifadhiwa) sasa ni mjamzito wa miezi 9, amesema kila siku alikuwa akibakwa na wanaume wapatao 40, na walikuwa wakifanya hivyo kwa zamuzamu na alipojaribu kukataa alimwagiwa maji ya moto.

“Kuna kipindi nilitakiwa nichague kati ya kifo na kulazimishwa kuafanya mapenzi, lakini vyote ilikuwa sawa na kifo hivyo niliwaambia wafanye wanachokitaka”, alisema msichana huyo.

Wasichana na wanawake wa Kiyazidi wanalazimishwa kufuata misingi ya dini ya kiislamu, na wakikataa wanakutana na adhabu kali ya kubakwa au kuuliwa, kitendo kinachowafanya wengi wakimbie nchini mwao.

Habari zinaeleza wapiganaji wa ISIS wameshaua wanawake na wasichana wengi jamii ya Yazidi, huku wengine wakiwakamata na kuwafanya watumwa kwenye kambi zao.

Nchi ya Syria imekumbwa na machafuko ya kisiasa kwa takribani tangu miaka mitano iliyopita ambapo baadi ya raia wanapinga uwepo wa madarakani kwa Rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad , na machafuko hayo sasa yanapelekea vita ya wenyewe kwa wenyewe huku udini ukianza kuchukua nafasi.

Apr 26, 2015

Hongera kwa family ya H Baba..kupata mtoto wa pili,anaitwa AFRIKA

Good Good NEWS.. YES, nimepita kwenye ukurasa wa H Baba Instagram, amepost picha ikiwaonesha wakiwa na mtoto wao mchanga halafu kaandika hivi”Uyu mimtoto wapili mke wangu anajifungua nashuhudia MWANZO wauchungu mpaka kijifungua kwake #Kiukweli heshima kubwa kwa mama Tanzaniteone ulijitahidi sana nakupa #HongeraKwakweli wewe nishujaa nanimfano wakuigwa Kwakweli kunamuda Nilikuwa nashindwa kavumilia natamani nitoke nje ila NASEMA hapana mpaka nishuhudie #mwisho wake!!!! ASANTE SANA “@h_baba123

H Baba ana mapenzi na Afrika yake.. mtoto huyu aliezalliwa tayari kapewa jina la Africa.. wa kwanza anaitwa Tanzanite.

Apr 21, 2015

Wastara anusurika kifo kwa ajali ya 9 kuwahi kupata

Msanii wa filamu, Wastara Juma amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari. Hiyo ni ajali yake ya 9 kuwahi kupata.

Wastara amewahi kupata ajali ya gari iliyomlazimu akatwe mguu wake.

“Dua zenu muhimu sana kwa mbao mnaonipenda na msionipenda,” ameandika kwenye picha aliyoweka Instagram inayomuonesha akiwa na jeraha usoni.

“Hali hii imenichosha sana ya matukio ya ajali kila mara natamani kuwa na amani na maisha yangu couz mungu ana sababu kuniacha niendelee kupumua mpka leo ila kwa wanaochukia kuona napumua wanatamani nizikwe hta mzima ila mtambue nina watot 3 wananitegemea kwa kila kitu smtime mnasema nasikitika sana ni kweli sababu mi sio nabii,” aliongeza.

“Nikihesabu hii ni ajali ya ya 9 sasa tena ni mbaya sana za kufa kabsa ila labda nimo kwa wale wanaopta ajali kipindi hiki japo kwangu ni too much,, ni jana na leo napumua alhamdulilah duwa zenu niombeni jamani huyu jinamizi akae mbali nami daah too much.

Apr 20, 2015

Diamond azungumzia ujumbe alioandika Wema Sepetu kuhusu tatizo lake la kutopata mtoto!

Kwa muda mrefu, Diamond Platnumz alikuwa akilijua tatizo la mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu la kutoshika mimba.
Akiongea na kipindi cha Ng’ari Ng’ari cha Clouds TV, Diamond alisema wakati wako pamoja waliwahi kuzunguka kwa wataalam mbalimbali kujaribu kupata tiba lakini hawakufanikiwa.

Alisema ilifika wakati alimweleza tu kuwa akubali hali hiyo.

Kuhusu kile Wema alichokiandika kwenye Instagram hivi karibuni ambapo alieleza ukweli wa hali yake ya kutopata mtoto, Diamond alisema ujumbe huo ulimuumiza kama wengine walivyoumia.

Alisema alikuwa anafahamu jinsi watu wanavyomshambulia Wema kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutopata mtoto na amemsifia kwa kuusema ukweli.

Hata hivyo aliwashauri watumiaji wa mtandao ya kijamii kuitumia vyema na sio kuitumia kuwatusi mastaa wao kwakuwa ni kweli maneno yao huwaumiza kama binadamu wengine.

Tweets 6 za Waziri Bernard MEMBE zenye majibu ya kinachoendelea South Africa..

Ishu ya mashambulizi ambayo yametokea Afrika Kusini imechukua HEADLINES kwa zaidi ya wiki moja.. labda hakuna aliyetegemea hali hii kujirudia, sio mara ya kwanza kuona wageni wakishambuliwa Afrika Kusini.. Picha na Video ziko nyingi Whatsapp zinaonesha watu wanauawa, wengine wanaumizwa.


Hizi ni Tweets sita za Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameandika kuhusu hali inayoendelea Afrika Kusini.


Apr 11, 2015

Huenda haya hukuwahi kuyasikia toka kwa Diamond Platnumz… Yako hapa #Hekaheka

Kwenye Leo Tena alikuwepo Diamond Platnumz pamoja na meneja wake, Babu Tale.. kama kawaida ya show ya Leo Tena pale huwa ni story nyingi nyingi zinakuwa zinaendelea, lakini Diamond nae akashea na watu wake kuhusu HEKAHEKA aliyowahi kukutana nayo.
Kulikuwa na maswali pia ambayo ilibidi Diamond ayajibu, mengi yalitoka kwa wasikilizaji wa show hiyo.


Ikaulizwa kuhusu tetesi za yeye na Meneja wake Said Fella kuwa na ugomvi, kisa vijana wa Yamoto Band hawajanunuliwa magari? Jibu la Diamond ni hapana.. hakuna ugomvi wowote, Babu Tale akasema mipango ya Management yao ni kufanya mengi mazuri kwa vijana wa Yamoto Band.. HAKUNA UGOMVI!


Likatupiwa swali la umri wa mpenzi wake Zari je? akajibu kwamba ni miaka 34 tu.

Ikaja sasa time ya kusikiliza Hekaheka aliyowahi kukutana nayo wakati anaanza muziki.. amesema alikuwa anapenda sana kuimba wimbo wa Z Anto wa ‘Binti Kiziwi’ .. wengine waliamini yeye ndio Z Anto mwenyewe, ikatokea msichana akampenda akijua anayempenda ni Z Anto.. baada ya video ya Z Anto kutoka watu wakamjua kwamba sio yeye ilibidi asiendelee kukatisha maeneo hayo.


Wengine waliuliza kama wimbo wa ‘Nasema Nawe’ ni wimbo alioimbiwa mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu..  nalo Diamond kalijibu, amesema huo wimbo hajaimbiwa Wema.. Ila aliuimba wakati akiwa na Wema… Hiyo ni burudani ambayo imezoeleka na wanawake wa uswahilini kwa hiyo kaona nao awaimbie.Amekataa kuwa na ugomvi wowote na Ommy Dimpoz, na wala hajawahi kukutana na Wema tangu walipoachana.
Kuhusu ujauzito wa Zari, Diamond amesema anatarajia mtoto mwezi wa saba au wa nane hivi.

ACHINJA MTOTO WAKE KAMA KUKU,"ADAI KAOTESHWA NA MUNGU"


Mchungaji akiwa chini ya ulinzi.
 DUNIA ina mambo! Mchungaji wa kanisa moja mjini Harare nchini Zimbabwe, ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, amekamatwa na polisi baada ya kukutwa akitaka kumuua mwanaye wa kumzaa kwa kumchinja na kisu shingoni, kitendo alichokifanya nyumbani kwake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mchungaji huyo ambaye hata hivyo hakueleweka ni wa kanisa gani, akiwa amevaa nguo zake za kichungaji, kanzu nyeupe yenye msalaba kifuani, alimchukua mwanaye huyo wa kiume na kuanza kumchinja ndani ya nyumba yake, kabla ya kijana huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kumi, kupiga kelele za kuomba msaada.

Kwa mujibu wa mitandao, baada ya majirani kuingia ndani ya nyumba hiyo, walimkuta mchungaji huyo akiwa na kisu mkononi, ameloa damu huku kijana wake akiwa ameanguka chini akiugulia kwa maumivu makali.

Baada ya kuhojiwa sababu za kutaka kutoa roho ya mwanaye, mchungaji huyo alitoa majibu ya kushangaza;

“Nilioteshwa na Mungu, Mkuu wa majeshi. Alinitaka kumtoa sadaka mtoto wangu kama kweli nilikuwa na imani naye, sasa kwa sababu kila siku hufanya mambo yangu kwa kusikia sauti yake, nikaifuatisha. Ni kama Ibrahim alivyofanya katika Biblia.”

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kijana huyo alikuwa bado hajafariki na aliwahishwa hospitalini ambako anaendelea na matibabu wakati mchungaji huyo ameendelea kuwa mikononi mwa polisi ambao wanamhoji kabla ya kufikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.