May 6, 2013

BIFU LA JAYDEE NA CLOUDS SASA LAFIKIA PABAYA, RUGE AAMURU CLOUDS KUTOPIGA NYIMBO YOYOTE YA BONGOFLEVA.......Akizungumza kupitia kipindi cha Power Breakfast, Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameelezea yafuatayo kuhusiana na tuhuma

zilizotolewa na msanii Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ wiki iliyopita:
Asema vita ya Lady Jaydee ameielekeza sehemu isiyo sahii kama tatizo ni Bendi ya SkyLight basi apambane kuipiku bendi hiyo na si kugombana na watu wengine.
Awaasa wasanii kukubali kupokezana vijiti na kujiandaa kwa maisha yajayo
Aelezea Clouds ilipomtoa Jaydee mpaka sasa alipo. Aaamua siku ya leo kutopigwa muziki wa Bongo Flava
Asema kuwa Clouds ni chombo binafsi kina maamuzi ya kufanya chochote pasipo kuvunja sheria
Asema siyo vizuri watu kuchafuana katika mitandao ya kijamii, kama kuna tatizo ni vyema kuonana na muhusika ili kumaliza tatizo