May 3, 2013

"BILA CONDOM HUWEZI KULIFAIDI PENZI LANGU HATA UKINIHONGA MABILIONI"...SHILOLE ..Mwigizaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Zena Mohamed, maarufu kwa jina la shilole amedai kuwa anaweza kufanya ujinga wowote humu duniani lakini linapokuja suala la mapenzi kamwe hawezi kwenda pekupeku ( bila condom ) ....

Akiongea kwa kujiamini ,Shilole alisema kuwa hata mtu awe vipi, au awe wa dini gani au awe na pesa kiasi gani kamwe hawezi kumvulia nguo kama hana kondom mkononi.....

Msanii huyo alienda mbali zaidi na kuzilaani kauli za baadhi ya watu zinazosema eti ukitumia "CONDOM" ladha ya mapenzi inapungua.Yeye anadai kuwa ni mdau wa "GEMU" hilo na huwa anatumia NDOM kama kawa na hufurahia kama kawaida...

" Hata niwe nimelewa kiasi gani huwa nipo makini sana maana najua vijana wengi wa mjini wananimezea mate....Waje tu , lakini bila KINGA wataambulia PATUPU!!” Alisisitiza Shilole