May 6, 2013

KANISA KATOLIKI LALIPULIWA NA BOMU JIJINI ARUSHA WAKATI MISA IKIENDELEATaarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba bomu limelipuka katika kanisa katoliki, parokia mpya ya Olasisi iliyokuwa inazinduliwa leo jijini arusha.....

Bomu hilo limelipuka wakati waumini wa kanisa hilo wa wakijiandaa na misa ya uzinduzi wa parokia hiyo....

Mpaka sasa haijajulikana idadi kamili ya watu waliojeruhiwa ama kupoteza maisha lakini taarifa za awali zinasema kuwa baadhi ya majeruhi wamekimbizwa hospitali

Chanzo cha mlipuko huo inasemekana kuwa kuna gari ndogo ilifika kanisani hapo na kusimama....

Baadae alishuka mtu aliyekuwa amevalia vazi mithili ya kanzu na kurusha kitu kuelekea kanisani ambacho ndicho kilichosababisha mlipuko huo..

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni balozi wa Vatican nchini Tanzania.Yupo baada ya kunusurika katika mlipuko huo

Hizi ni taarifa za awali tu. Taarifa kamili itawekwa itakapopatikana. Tafadhali endelea kusikiliza Redio Maria Tanzania (inasikika pia online muda huu wakiwa wanatangaza kuhusu tukio hili )