May 6, 2013

MWANAMKE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR
Majambazi yamempora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi na kutokomea kusikojulikana....

Tukio hilo limetokea leo saa 5:16 jioni na inavyosemekana ni kuwa mwanamke huyo alikuwa akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia..

Alipotoka ,majambazi hayo yalimfuata na kuligonga gari lake makusudi na ndipo dada huyo aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa. ..