May 30, 2013

PICHA KIBAKA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUMCHANA WEMBE WA MGONGO ASKARI POLISIKijana ambae ni kibaka na ahakufahamika jina lake akisurubiwa na wana usalam baada ya kuchana na wembe Askari Polisi aliyekuwa uwanjani kwenye shoo ya Open Mic iliyofanyika kwenye viwanja vya Temeke Mwembe Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kijana aliomba ardhi ipasuke kwa kipigo kikali ambacho hakika bila na nguvu za giza watu wangesimulian


Na Livingstone Mkoi

Kijana asiyejulikana jina lake hivi karibuni alionja joto ya jiwe kwa baada ya kuchezea kipigo cha mbwa mwizi toka kwa wanausalama waliokuwa uwanjani kufuatia kumjeruhi Askari Polisi kwa kumchana na wembe mgongoni wakati askari huyo akimkamata mmoja wa vibaka hao.

Hata hivyo kutokana na wingi wa vibaka ambao ni wazoefu wa eneo hilo walipambana vya kutosha na wana usalama.Hata hivyo wakati wanausalama hao wakijaribu kumkamata mmoja wa vibaka waliokuwa wanapora wananchi ndipo kibaka mmoja anaeonekana pichani alipojitoa muhanga na kumchana kwa wembe Polisi.

Baada ya tukio hilo kijana huyo alikamatwa na kuanza kuchezea kichapo cha nguvu,huku polisi huyo akikimbizwa Hospitali kutibiwa.