Jun 1, 2013

KIJANA ANUSURIKA KIFO BAADA YA VIBAKA KUMCHOMA MOTO.TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI


  Kijana mmoja alietambulika kwa jina la Ismai Mayoba(31)anaefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Jamhuri Manispaa ya Lindi amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo.


Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo
lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.


Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndugu Ally Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie Moto huku akijua ni kosa kisheria.Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo


Taarifa zaidi tutawaletea kuhusiana na tukio hilo.