Jun 3, 2013

LADY JAYDEE NA T.I.D WASAMEHEANA BAADA YA KUZINGUANA KISA SHOW YA JIDEWakati mwingine matatizo hukutanisha watu waliokosana na kuufufua tena urafiki wao. Harakati za maandalizi ya mazishi ya marehemu Albert Mangwea zimewakutanisha marafiki wawili walioingia kwenye tofauti hivi karibuni, Lady Jaydee na TID.

Hivi karibuni TID alitangaza kujitoa kwenye show ya miaka 13 ya Jaydee na kuweka sababu tatu. Kutokana na uamuzi huo wa TID, watu walimchukulia kama msaliti kwa Jide aka Anaconda waliyewahi kufanya hit ya pamoja, Understanding.

Hata hivyo Jaydee amesema alikutana na TID kwenye kamati ya mazishi ya Mangwea na kuweka tofauti zao pembeni.

“I met TID kwenye kikao cha msiba wa Ngwair. I love him, forgive him, he’s ma frnd ana matatizo yake pia but not naniliu,” ametweet Jide.