Jun 25, 2014

KAJALA: SINA HAMU YA KUISHI BONGO

Ohoo! Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amefunguka kuwa yuko Bongo kwa kuwa ndipo nyumbani kwao lakini hana hamu ya kuendelea kuishi nchini kutokana na kuzushiwa mambo kila kukicha.

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko wikiendi iliyopita, mwigizaji huyo alisema anapenda awe na maisha ya furaha na wanawake wenziye kwa kubadilishana mawazo ya hapa na pale lakini kwa sasa hana upendo huo kwa kuwa kuna watu wanaishi kwa kutegemea bifu.
“Unajua inauma sana, unaenda klabu unamkuta mtu ambaye huko nyuma alikuwa shoga’ko, kula, kuvaa na kila aina ya ushirikiano mnapeana, sasa mnakuja kugombana, kiukweli roho huwa inauma ndiyo maana nashindwa hata kwenda klabu kuepusha mengi, nasubiria viza yangu itoke nisepe zangu China,” alisema Kajala.Kwa muda mrefu kumekuwa na ugomvi usiokwisha kati ya Kajala na mwigizaji mwenzake, Wema Sepetu

0 comments:

Post a Comment