Jun 28, 2014

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA ASKARI POLISI KITUO CHA POLISI KIMANZICHANA AKAMATWA HUKO ZANZIBAR


Jeshi la polisi Zanzibar limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa mauaji ya askari wa polisi na mgambo mmoja ambao waliuwawa kwenye tukio la uvamizi wa kituo cha polisi cha Kimanzimchana  walaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani Juni 11 mwaka huu.

Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi wa mkoa wa Kusini Pemba  ACP  Juma Yussuf Msige amemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la Hamis Othman Mzee maarufu kwa jina la Hamis Mabunduki  na makachero walifanikiwa baada ya kufuatilia nyendo zake na kumkamata  wakati wa mchana akiwa mafichoni katika kijiji cha Matale Chake Chake Pemba na hivi sasa wanawasilaina nawenzao wa Pwani kwa ajili ya upelelezi zaidi.

0 comments:

Post a Comment