Jul 27, 2014

Shilole Atangaza Kugombea Ubunge Jimbo La Igunga 2015.

Muigizaji wa filamu na mwanamuziki Shilole ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Igunga anakotokea katika uchaguzi mkuu ujao 2015. Shilole ameyasema hayo jana kupitia kipindi cha Sizi za Kitaa cha Clouds TV huku ile collabo yake na Jennifer Lopez wa Marekani ikiwa bado inasubiriwa na mashabiki wake.

"Baada ya Dr. Dalali Kafumu anayefuata ni mimi, mimi nadhani napenda jimbo langu na napenda wakazi wangu wa Igunga wananiona toka nakua mpaka sasa hivi, kwahiyo wanafurahi, sasa wananiambia sisi hatutaki kumpa mtu mwingine kiti hiki sasa wananipa changamoto. Vitu viwili vya kwanza ambavyo nitavifanya nikiingia kwenye lile bunge nikiwa kama msanii kwanza natetea haki za wasanii, cha pili Igunga yangu wapo wakazi vijana wapate kazi, yaani akina mama, wale mama lishe na wengine lazima wawe na kazi zao. kwahiyo nitawatafutia kazi. nitajenga chuo cha muziki" alisema shilole

"Mimi jimbo langu nalijua na nimekulia pale mpaka nimekuwa mkubwa lazima nilitimize sitaki wananchi wangu wapate tabu. mimi nadhani wanaoenda kugombea majimbo yasiyo ya kwao wanaweza kufanya chochote lakini kama wewe ni mzaliwa wa hapo itakuuma, lakini unakuta mtu wa Dar es salaam anakwenda kugombea Mtwara huko nani anamjua? mimi nitaenda kugombea kwangu lazima nitapata kura lazima watanipa ! kwa hiyo kaeni ytayri Shilole ni mbunge mtarajiwa" alijitapa Shilole

0 comments:

Post a Comment