Aug 15, 2014

DIAMOND AMPIGA VIJEMBE WEMA SEPETU

STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amemtupia vijembe mpenzi wake Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram akionekana kuchukizwa na tabia ya staa huyo kupenda maisha ya starehe zisizo na faida.



Katika ujumbe huo, Diamond ameandika kuwa angewaona mashabiki wa mrembo huyo wana akili na mapenzi ya dhati kama wangemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na kuacha starehe zisizo na faida na kutumia fedha kufanya mambo ya maendeleo kuliko kuvifaidisha viwanda vya kutengeneza pombe.

0 comments:

Post a Comment