Sep 6, 2014

HABARI YA KUSIKITISHA: AJALI YAUA ZAIDI YA 50 MUSOMA NI MABASI YA MWANZA COACH NA JUMANNE, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA
 Mabasi hayo yakiwa yamegongana


Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Butiama ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo Anjelina Mabula aliyezungumza na TBC muda mfupi uliopita amesema ajali hiyo imehusisha basi la AM Coach lenye namba za usajili T736 AWJ likitoka Musoma kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi T677 CYC J4 Express likitoka Mwanza kwenda Tarime na gari jingine dogo aina ya Nissan Corola P332 KKT likitoka eneo la Sabasaba yote yalikutana kwenye mteremko yakitokea juu kwenda Darajani katika kupishana ,kutokana na spidi waliyokuwa nayo hawakuweza kupishana yakagongana na wakati huo gari dogo likapaki pembeni nalo likagongwa kwa nyuma likasukumwa na kutumbukia mtoni.

Katika gari dogo watu wawili wamefariki dunia na majeruhi 36 kutoka kwenye mabasi nao wamefariki na majeruhi 80 wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mara.

Madereva wote wamefariki dunia,na kwamba mizigo ya majeruhi iko chini ya ulinzi wa polisi


Basi la Jumanne lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza coach lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Musoma. Ajali imetokea katika eneo la daraja la sabasaba, Musoma.

0 comments:

Post a Comment