Sep 6, 2014

Mark Hughes: Sijafahamu Peter Osaze Odemwingie Hatocheza Kwa Muda Gani

Mshambuliaji kutoka nchini Nigeria na klabu ya Stoke City, Peter Odemwingie itamchukua muda mrefu kurejea tena uwanjani baada ya kubainika ameumia vibaya sehemu za goti la mguu wa kulia.

Meneja wa klabu ya Stoke City, Mark Hughes amethibitisha taarifa za mshambukliaji huyo kutarajia kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kijacho, ambapo amesema ni huzuni kubwa kwake kumkosa Odemwingie kwa muda mrefu kutokana na kutambua umuhimu alionao kwenye kikosi cha The Potters.

Hughes, amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa mkia 33, alifanyiwa vipimo mwanzoni mwa juma hili na imebainika aliumia vibaya sehemu za goti lake la mguu wa kulia wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Man city ambao walikubalia kulala nyumbani kwa bao moja.

Amesema kutokana na majibu kuonyesha hivyo, jopo la madtari klabuni hapo limeshauri Odemwingie afanyiwe upasuaji ili kuharakisha hatua ya kupona jeraha hilo ambalo lilionekana kumsikitisha kila shabiki wa Stoke City, ambaye alimuona mshambuliaji huyo akiugulia huko Etihad Stadium.

Hata hivyo Hughes, ameshindwa kuweka wazi ni kipindi cha majuma ama miezi mingapi ambayo itapita kwa mchezaji huyo bila kucheza soka, kutokana na uhalisia wa tatizo linalomkabili kwa sasa.

"Sina budi kusema suala la kukaa kwake nje ya uwanja halifahamiki kwa sasa itategemea na upasuaji atakaofanyiwa siku za hivi karibuni, lakini niaamini haiwezi kuwa kipindi kirefu sana.” Amesem Hughes.

"Ni taarifa ambazo zimemshtua kila mmoja wetu kwa sababu tulihitaji kumuona mshambuliaji Odemwingie akiichezea Stoke hadi mwishoni mwa msimu huu kwa mafanikio makubwa, lakini kilichotokea tunalazimika kukubaliana nacho na kutazama mambo mengine kuendelea kikosini.” Amongeza Hughes.

Peter Odemwingie alijiunga na Stoke City katika majira ya kiangazi akitoke Cardif City baada ya klabu hizo mbili kukubaliana kubadilishana wachezaji ambapo kwa upande wa The Bluebirds walikubali kumchukuwa mshambuliaji kutoka Trinidad na Tobago Kenwyne Joel Jones.

0 comments:

Post a Comment