Sep 26, 2014

Sio Lazima Nijue Kiingereza Hata Messi Hakijui: Ray

Vicenti Kigosi akichat Live na mashabiki katika ukurasa wa facebook wa EATV.
Mkurugenzi wa Kampuni ya filamu Rj Company,Vicenti Kigosi amesema si lazima kujua Kingereza maana hata Messi hajui, Ray amesema hayo alipokuwa akichat Live na mashabiki zake kupitia ukurasa wa Facebook wa East Africa Television katika kipengele cha Kikaangoni Livekinachokukutanisha na watu mahiri kila siku ya jumatano kuanzia saa sita za mchana mpaka nane kamili.


SI LAZIMA NIJUE KIINGEREZA
Mkali huyo ambae kwa sasa anachukuliwa kama moja ya watu wenye mafanikio katika tasnia ya filamu nchini ambae pia ameshawishi vijana kibao kuingia katika tasnia hiyo amefunguka na kuweka wazi kuwa suala la lugha ya kiingereza kwake ni changamoto lakini si jambo la ajabu sabgabu kuna watu wengi maarufu duniani wanapigwa chenga na lugha ya kiingereza.Prince Dully >>>>Mbona haujui kingereza au uliishia darasa la saba,nini?
RAY Kigosi >>>>>>Hata messi hajui kiingereza kwani mimi muingereza nijue Kiingereza.


CHUCHU MCHUMBA WANGU
Msanii Vicent Kigosi ambae katika hizi siku za karibuni ilisikika kuwa yupo katika mahusiano na msanii mwingine wa filamu ambae anafahamika kama Chuchu Hansi hivyo ilipelekea mashabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV kutaka kujua ukweli juu ya mahusiano hayo na kama kweli jamaa anampango wa kumuoa binti huyo au laah,na majibu ya Ray uyalikuwa kwamba wawe watulivu muda utakapofika ndio watajua ukweli wote juu ya suala hilo.


Ronald Robert >>>> Utamuoa chuchu hansi au ndio kuchezeana tu?
RAY Kigosi >>>> Muda ukifika utajua kila kituLakini mbali na mashabiki kuwa na mtazamo tofauti juu ya maisha yake ya mahusiano Ray amekubali moja ya ushauri aliopewa na shabiki mmoja kuwa huu ni wakati wa yeye kuoa na kuwa katika ndoa yenye heshima kwa kuwa umri wake kwa sasa umekwenda.


Fabian John >>>>>Bwana Kigosi ni vizuri ukaoa na ukawa na ndoa yenye heshima kwan wewe ni mtu mkubwa.
RAY Kigosi >>>>>Ushauri ni mzuri sana nitaufanyia kazi.AKANA KUWA FREEMASON
Vinaja wengi wamkekuwa na dhana potofu pindi kijana mwenzao anapopata mafanikio ya haraka au kufanikiwa katika maisha wamekuwa wakiwahusisha watu hao na imani ya Freemason ambayo kwa mujibu wao wanahisi mtu akiwepo katika imani hiyo anafanikiwa kwa haraka na mambo yake yanakwenda safi,hivyo moja ya shabiki alitaka kujua kama yale yanayozungumzwa mtanii ni kweli na hapo ndipo Ray Kigosi alipokana kuhusika na imani hizo za Kifreemason.


KANUMBA ALIKUWA MSHINDANI WANGU.
Vicenti Kigosi amefunguka na kuweka wazi kuwa Marehemu Kanumba alikuwa ni rafiki yake wa karibu na ni mtu ambae alikuwa anampa changamoto katika masuala ya kimaendeleo na kumfanya kusogea mbele zaidi kimaendeleo lakini mkali huyo anasema toka alipofariki Kanumba amekuwa akikosa tena na kumiss ule ushindano wao ambao ulikuwa ukimfanya apige hatua mbele katika maendeleo.
"Ni vitu vingi sana namkumbuka mshikaji wangu Kanumba hasa ni ushindani wangu na wake kwa upande wa maendeleo jambo ambalo lilikuwa linafanya tusonge mbele kimaendeleo" hivyo huu ulikuwa ni ushgindani wa kimaendeleo maana mwenzako anapofanya jambo fulanai wewe unatamani kufanya kama yeye au kufanya kubwa zaidi yake hivyo huwezi kusema hili lilikuwa bifu,hivyo sijawahi kuwa na bifu nae ila tulikuwa tukishindana kimaendeleo."


SINA MAHUSIANO NA JOHARI
Ray amekana kutoka kimapenzi na msanii Blandina Chagula na kuwa mtaani kuna habari nyingi sana na nyingi hazina ukweli lakini kwa kuwa sisi ni kioo cha jamii hivyo jamii inakuwa inatuzungumzia kwa mambo mengi sana lakini ukweli ni kwamba sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Johari na wala sijawahi kuweka wazi juu ya maisha yangu ya mapenzi bali baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikizusha na kudanganya umma lakini Johari ni Mkurugenzi mwenzangu katika kampuni yetu na sii mpenzi wangu wala si mchumba wangu

0 comments:

Post a Comment