Oct 27, 2014

Amwagiwa uji wa moto na mke wa bosi wake, kisa kuhisiwa kuchepuka na bosi wake

MSICHANA mmoja mkazi wa eneo la Minga katika Manispaa ya Singida (muuza duka), amenusurika kifo baada ya kumwagiwa uji wa moto na mke wa tajiri yake na kumsababishia maumivu makali kutokana na kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya mkoa wa Singida, wodi namba mbili ya wanawake, Anna Sprian ameifahamishakuwa binti huyo amejeruhiwa sehemu za sikio la upande wa kulia na mgongoni, ambapo amesema hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri kutokana na matibabu anayoyapata hospitalini hapo.


Akizungumza Agosti 10, 2014 kwa tabu, binti huyo Jackline Lasway (23), maarufu kwa jina la Pendo, amesema majeraha ya moto katika sehemu ya sikio la upande wa kulia na mgongoni.

0 comments:

Post a Comment