Oct 29, 2014

Hatimae Chid Benz amepata dhamana.

Taarifa ambazo zimetoka muda mfupi uliopita zinasema kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ asubuhi ya leo October 29 amepata dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyotolewa.

Chid Benz alipandishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jana October 28 na kusomewa mashtaka matatu yaliyokuwa yakimkabili ambapo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Leo asubuhi amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kesi yake ya kukamatwa na dawa za kulevya,kesi yake inatarajiwa kusikilizwa tena October 11 mwaka huu 2014.

Source:Globalpublishers.com

0 comments:

Post a Comment