Oct 9, 2014

Huu sio msafara wa kiongozi, ni wa mtu aliekutwa na Ebola Huko Hispania

Kuna Nesi mmoja amegudulika kuwa na ugonjwa wa Ebola baada ya kuwahudumia Wamishionari wawili waliokua na ugonjwa huo baada ya kutoka nao Sierra Leone walikokua wamekwenda kujitolea kufanya kazi.

Ugonjwa wa Ebola imekua ishu kubwa kwenye hizi nchi maarufu duniani ambazo zimejikuta zikiingia kwenye headlines baada ya Wagonjwa kuanza kugundulika ambapo Marekani kuna mmoja aliingia na Ebola kutokea Afrika na mwingine ni huyu Nesi wa Hispania.
Labda unaweza kushangaa ni jinsi gani huyu Nesi amekua akilindwa baada ya kujulikana amepata huo ugonjwa, hiyo picha ya juu sio msafara wa Kiongozi bali ni Polisi walikua wanamsindikiza Nesi huyo kumpeleka Hospitali ya Carlos III.Hawa ni Wafanyakazi nje ya hospitali ya La Paz University wakiwa wameungana pamoja kutoka Waziri wa Afya wa Hispania Ana Mato ajiuzulu baada ya mgonjwa wa Ebola kugundulika.
Baada ya kuugua Ebola Nesi huyu ambae bado jina lake wala sura yake havijaonyeshwa alisababisha Mume wake pamoja na watu wengine 50 kuwa chini ya uangalizi ili kujua kama na wao wameambukizwa lakini mpaka Jumanne jioni (October 7) hakuna yeyote kati yao aliekutwa na Ebola.Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Mwanaume wa Nigeria ambae aliingia Hispania siku kadhaa zilizopita pia alichukuliwa na kuchunguzwa lakini hakukutwa na Ebola, vivyo hivyo kwa Nesi mwingine ambae alikua akifanya kazi na Nesi wa kwanza aliekutwa na Ebola, baada ya kuharisha aliwekwa chini ya uchunguzi lakini ikagundulika hakuwa amepatwa na Ebola.

0 comments:

Post a Comment