Oct 9, 2014

Kajala na Wema watoana jasho polisi
Stori: Waandishi Wetu
Kufuatia matusi ya mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu kwenda kwa mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, mastaa hao wamejikuta wakitoana jasho kwenye
Kituo cha Polisi cha Kijitonyama almaarufu Mabatini jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.Mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’.

DURU ZA ‘KIUBUYU’
Duru za ‘kiubuyu’ zilidai kwamba Kajala, baada ya kuchoshwa na matusi hayo ambayo yalianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Wema, alijikuta akiishiwa na uzalendo kisha kuingia mzigoni ili kukomesha matusi hayo kwenye mitandao ya kijamii.

MATRIDA MBARONI
Ilidaiwa kwamba, Kajala akiwa na timu yake (Team Kajala) alifanikiwa kumtia mbaroni dada mmoja aliyetajwa kwa jina la Matrida akidaiwa kwamba ni mfuasi wa Wema (Team Wema).
Ilisemekana kwamba Matrida anayetumia jina la ‘Mat Kiboko Yao’ kwenye ukurasa wake wa Instagram ndiye ambaye amekuwa akiongoza jahazi la kumtusi Kay.
Ilizidi kunyunyizwa kwamba sakata hilo la kuanikwa Instagram lilianza siku mbili baada ya ile pati ya kuzaliwa ya Wema ambapo Mat Kiboko Yao alimtukana Kajala matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini) kupitia ukurasa wake kwenye mtandao huo.

KAJALA ACHOKA, AKIMBILIA POLISI
Ilidaiwa kwamba Kajala alipoona amechoka kutukanwa, alitafuta wataalam ili kujua namna ya kumkamata na alipomjua ndipo akakimbilia Kituo cha Polisi cha Mabatini kwenda kutoa taarifa.
RB

Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu.
Gazeti hili lilifanikiwa kunasa namba ya jalada la kesi hiyo iliyosomekaKJN/RB/8854/2014-MATUMIZI YA MATUSI MTANDAONI.
Ilisemekana polisi walitumia mbinu zao na kufanikiwa kumkamata Mat Kiboko Yao na kumweka nyuma ya nondo za mahabusu kituoni hapo ndipo sarakasi za pande mbili zikaanza.


KWANZA
Mara tu baada ya Mat Kiboko Yao kukamatwa mishale ya saa 2:00 usiku, taarifa zilisambaa kama moto wa kifuu ndipo Team Wema ikaingia mzigoni kutaka kumtoa mwanadada huyo lakini wakagonga mwamba.


WEMA, PETIT MAN WATINGA MABATINI
Ilidaiwa kwamba, baada ya Mat Kiboko Yao kutiwa mbaroni, Wema na jeshi lake akiwemo Petit Man walitinga Mabatini kwa ajili ya kumtoa mwanadada huyo lakini aligonga mwamba na kumuacha akilala kituoni hapo.
“Yaani ulikuwa ni usiku wa kutoana jasho na kupimana ubavu kwamba nani ni nani. Ilikuwa akitoka Kajala kuhakikisha kwamba mtuhumiwa wake aachiwi, Wema naye anatinga kituoni kwa mbwembwe kutaka Mat Kiboko Yao aachiwe kwa gharama yoyote.
“Hapo ndiyo ngoma ilikuwa nzito, kila mmoja alikuwa anamuonyesha mwenzake kuwa ni zaidi na ni maji marefu hadi kulipokucha muvi likaendelea,” alisema shuhuda aliyefuatilia sakata hilo kinagaubaga.


Mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu.


WAANDISHI WAPEWA UBUYU, WATINGA MABATINI
Kulipokucha, waandishi wetu walipewa ubuyu huo ndipo wakatinga Mabatini kisha wakatega ‘rada’ zao na kuweka doria.
Wanahabari wetu, wakiwa kituoni hapo walimshuhudia Kajala akilinda kituoni hapo asitokee mtu yeyote akamtoa Mat Kiboko Yao.
Hata hivyo, alipoulizwa Kay kulikoni kuwa eneo hilo alisema alikuwa ameitwa kwa ajili ya kusuluhishwa badala ya kupoteza muda kwa jambo kama hilo.


KAJALA NA KUNDI LAKE
Awali Kay alionekana akiingia kituoni hapo na kundi lake la watu watatu akiwemo mwanaume mmoja ambapo yeye aliingia mpaka kwenye chumba cha mkuu wa kituo.
Kajala akiwa kwa mkuu wa kituo, haikujulikana kilichokuwa kikiendelea ndani kwani kulikuwa na kikao cha muda mrefu ambapo ghafla Kajala na mtuhumiwa wake waliyeyuka.


WEMA AINGIA MITINI
Wakati hayo yakiendelea kituoni hapo, si Wema wala jeshi lake waliofika kwa ajili ya kumtetea Mat Kiboko Yao ambaye ndiye kiongozi wa Timu Wema kwa kutukana.
Hata hivyo, baadaye alionekana mmoja wa marafiki wa karibu ambaye ni ndugu wa Mat Kiboko Yao aliyekuwa akihaha kumtoa mwenzake.

TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni Mama Wema alimtolea uvivu Kajala na kumtusi ndipo akafufua upya kile kidonda cha Sh. milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kay asiende jela na kinachoonekana, bado fedha hizo ni tatizo kubwa.
Imeandaliwa na Hamida Hassan, Imelda Mtema, Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani.

Source: GPL

0 comments:

Post a Comment