Oct 29, 2014

MTANGAZAJI WA STAR TV ANUSURIKA KUFA,AJALI YA GARI
Mtangazaji wa Star Tv, Sauda Mwilima.


MUNGU mkubwa! Mtangazaji wa Star Tv, Sauda Mwilima amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Mlimani City jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita.

Ajali hiyo ilitokea katika mataa ya kuongozea magari yaliyopo maeneo hayo ambapo lori lilikosea njia na kugonga gari lake aina ya Toyota Ipsum na kuharibika huku mwenyewe akipata majeraha mkononi na kubanwa kifua.

“Kweli ajali ilikuwa mbaya lakini nashukuru Mungu bado ninapumua japo nimeumia mkono na kifua, gari limeharibika vibaya lakini naamini nitapata lingine au litatengenezwa, kikubwa bado napumua, namshukuru sana Mungu,” alisema Sauda

Muonekano wa gari hilo baada ya ajali

0 comments:

Post a Comment