Nov 10, 2014

HILI NDILO GONJWA LINALOMSUMBUA MR NICE KUTOTULIA KATIKA LABEL MOJA

Mr Nice amesema label nyingi zinashidwa kuelewana naye kutokana na wao kuhitaji sehemu kubwa katika kinachopatikana pamoja na kumnyima mamlaka kama msanii mkubwa.

Mwanzilishi wa mtindo wa TAKEU ambao haupo tena, Lucas Mkenda aka Mr Nice 


“Tumeshindwana kwa sababu ya utawala kwa sababu ukiangalia mikataba yangu yote wao ndo wanataka wawe mabosi, kitu ambacho kwangu hakiwezekani,” Nice ameiambia Bongo5. “Halafu unataka uni-meneji wakati kabla wewe kukutana na mimi nilishakuwa na kazi zangu nyingi ambazo bado zinahitajika. Wakati mimi bado nina jasho langu la Kikulacho, la Fagilia, album zangu ambazo mimi nimefanya mimi mwenyewe kwa jasho langu nikajipromoti mwenyewe iweje unimeneji halafu utake kupata asilimia kutoka kwenye jasho langu? Huoni huo ni wizi wa wazi wazi?
 Mr Nice akiwa kwenye nyumba yake iliyopo Kibamba jijini Dar es salaam
Candy & Candy mimi niliwaambia kazi yangu inaendelea kubaki kazi yangu ile ya nyuma, kama mnataka tutafanya project mpya ndo tutaongelea suala la percent gani mtapata kutokana na promotion mtakayoifanya lakini hamna uwezo wa kusimamia kazi yangu yote ambayo niliifanya kwa jasho langu. Kama niliweza kufika hapa nilipo sasa nahitaji menejimenti ya nini? Mbona niliweza kujitoa toka huko nilipokuwa mpaka nikafika hapa?,” amehoji.

“Mimi nadhani mikataba iliyovunjika ni miwili na sababu za kuvunjika zinafanana.. Nakumbuka nilikuwa na mkataba na akina Lamar tukashindwana hapo kwenye suala la nani ni nani katika mkataba, basi tukasema tuache mkataba mpaka uishilie huko. Nikafanya mkataba na GrandPa Records Nairobi ambayo nao tulishindwana kwa sababu hizo hizo. Unajua mara nyingi unaposhindwana mikataba na hawa watu wanazusha chochote. Sijui jamaa hataki kunisikiliza, jamaa anafanya hizi lakini ukweli unakuja pale pale, mameneja wanataka uwafuate wao wanataka nini, Mimi ninaimba muziki wa watoto wa uswahilini inakuwaje unataka nikawaimbie watoto wa Masaki? Mimi nadhani mameneja wengi wanakuwa wasanii kufanya vitu kwa mitazamo yao bila kuangilia na malengo ya msanii binafsi.”

0 comments:

Post a Comment