Nov 14, 2014

Kamati ya Miss Tanzania imeingia katika skendo ya kushindwa kukamilisha mahitaji ya Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa ili kwenda Miss World 2014

Miss Tanzania 2013/2014 Happiness Watimanywa
Kamati ya Miss Tanzania imeingia katika skendo nyingine ya kushindwa kukamilisha mahitaji ya Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa ili kwenda Miss World 2014 ambapo anatakiwa kuondoka weekend hii.
Mama mzazi wa Happiness Watimanywa akizungumza na E-Newz ya East African Television ameilalamikia kamati hiyo kwa ubabaishaji kwa madai imemlazimu pia kutoa mahitaji ya mwanae yaliyotakiwa kutolewa na kamati hiyo.

"Wanasema hiki wanasema hiki, kwa mfano kama introduction shooting wakasema kwamba is very expensive kwa hiyo mimi nikajitolea nikalipa milioni moja down payment, tangu mwezi wa tano nlikuwa nawaambia mpaka two weeks ago hawana jibu lolote, mimi naogopa mwanangu asije akashushwa kwenye stage, wewe huna visa hauruhusiwi kuja kushiriki shindano hili. Haya hela ya shopping ambayo ni shilingi millioni tano walipaswa wamlipe mtoto mpaka leo bado siku mbili mtoto anaondoka Jumamosi leo wanamkabidhi tiketi bado hawajampa hela ya shopping sasa mtoto anaendaje bila maandalizi?, ndiyo maana nchi yetu kila mwaka inakuwa ya mwisho" alisema mama HappinessHappiness akiwa na mama yake mzazi


Hili ni janga jingine la kamati ya Miss Tanzania baada ya sakata la Sitti Mtemvu kudanganya umri huku kamati hiyo ikionekana kumtetea kabla ya watanzania na mashabiki wa urembo kulivalia njuga mpaka Sitti yakamshinda na kulibwaga taji hilo lililoenda kwa Lilian Kamazima.

0 comments:

Post a Comment