Nov 5, 2014

Nabii Yaspi Bendera Amtabiria Sitti Mtemvu Kutwaa Taji La Miss World 2014 !

Nabii Yaspi Bendera wa kanisa la The Revelation Church amemtabiria Sitti Mtemvu kutwaa taji la Miss World 2014 licha ya kuandamwa na skendo ya kughushi umri wake.
Issue hiyo ilitokea baada ya mapaparazi wa Globalpublishers kwenda maeneo ya Buza Kipera lilipo kanisa hilo ambalo Sitti Mtemvu anadaiwa kuabudu hapo. Mapaparazi walienda kumuulizia Sitti Mtemvu ingawa waliambiwa ana muda kidogo hajaonekana. Ila Nabii Yaspi alisikika akimkingia kifua Sitti kuhusu kuandamwa kudanganya umri na kusema alistahili pia kushinda taji la Miss Tanzania 2014 na kuwaonya wanaomwandama
Sitti Mtemvu na Nabii Yaspi Bendera wa kanisa la The Revelation Church
"Mara ya kwanza nilimtabiria Sitti kushinda u-miss Tanzania na kweli akashinda, sasa wanatokea watu wakidai mara ana hipsi kubwa, ooh kadanganya umri, huu wote ni upepo tu na utapita.“Kama Sitti hatakengeuka kwenye imani yake atafika mbali zaidi na kushinda hata Miss World. Wale wote watakaoendelea kumfuatilia wataparalaizi"

0 comments:

Post a Comment