Nov 12, 2014

WADAU WAMTAKA SITTI AJIVUE TALI LA MISS CHANG’OMBE NA TEMEKE

Baadhi ya wadau wa sanaa waliozungumza na Risasi Mchanganyiko Jumatatu iliyopita jijini Dar walisema kama kweli Sitti ana dhamira safi ya kukwepa kusakamwa basi ni bora kwake akavua na mataji ya Miss Chang’ombe na Miss Temeke ambayo ndiyo yaliyompa tiketi ya kwenda kambi ya Miss Tanzania na kushinda.

Aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu.


Wadau hao walisema kuwa, sheria za Miss Tanzania zinaanzia vitongojini, wilaya, mikoa, kanda na hatimaye taifa kwa hiyo kama skendo ya kudanganya umri imemla mpaka akaamua kujisalimisha, basi bado hana sifa za kuwa Miss Chang’ombe na Miss Temeke wa mwaka 2014.

“Kwanza kabisa nasema Sitti hajavua taji la Miss Tanzania kwa sababu ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu kudanganya umri bali ni kweli amedanganya, anajijua.

“Kama angekuwa hajadanganya, kwa nini asitoe paspoti yake inayomwonesha ana umri wa miaka 23? Mambo yalimfika shingoni ndiyo maana. Anachotakiwa ni kuvua taji la Miss Chang’ombe na Miss Temeke mwaka huu,” alisema Ismail Chandu, mkazi wa Temeke jijini Dar.

Shindano la kumsaka Miss Chang’ombe lilifanyika Juni 27, mwaka huu kwenye Ukumbi wa TCC Chang’ombe, Dar ambapo Sitti aliibuka kidedea akifuatiwa na Paulina Elisante (anayetakiwa kuchukua taji), wa tatu ni Derena David.

Shindano la Miss Temeke 2014 lilifanyika Agosti 22, mwaka huu kwenye Ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe jijini Dar ambapo Sitti Mtemvu aliibuka kidedea akifuatiwa na Salama Saleh (anayetakiwa kushika nafasi ya kwanza) na nafasi ya tatu ilitwaliwa na Neema Mollely.

Novemba 5, mwaka huu, Sitti Mtemvu aliiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Hashim Lundenga akisema ameamua kwa hiyari yake kuvua taji hilo.Sitti alifikia uamuzi huo baada ya kuandamwa na skendo ya kudanganya umri wakati akigombea taji hilo
0 comments:

Post a Comment