Dec 2, 2014

Akaunti ya benki ya 50 Cent yashikiliwa!

50 Cent hawezi kutoa hata senti kwenye ATM, sababu akaunti yake binafsi ya benki imeshikiliwa.
Kwa mujibu wa TMZ, 50 hakuweza kulipa kiasi cha dola milioni 17.2, alizotakiwa kulipa kutokana na hukumu ya deal alilopewa la kutangaza headphones za kampuni iitwayo Sleek Audio.
Sleek ilidai kuwa 50 aliiba design yake na kujaribu kuzifanyia masoko yeye mwenyewe. Sheria iliwapendelea Sleek na 50 kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha.
Hata hivyo chanzo kilicho karibu na 50 kimesema anaweza kutumia akaunti zake zingine kwakuwa iliyoathirika ni yak wake binafsi. Pia, fedha iliyopo kwenye akaunti hiyo ni vijisenti tu kwakuwa Forbes ilimkadiria kuwa na utajiri wa dola milioni 140.

0 comments:

Post a Comment