Dec 15, 2014

KUHUSU MGOMBEA WA CCM KUFARIKI GHAFLA MUDA MFUPI BAADA YA KUPIGA KURA JANAMgombea uenyekiti kupitia CCM Mtaa wa Swea, Kata ya Mkolani, Nyamagana, Mwanza, Pius Mihayo (siyo pichani) amefariki dunia ghafla akiwa mtaani kwake, muda mfupi baada ya kupiga kura.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Halifa Hida alisema mgombea huyo alifariki dunia ghafla akiwa kwenye mtaa wake wa Swea na chanzo cha kifo hicho hakijajulikana...
Sasa kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi, tutatangaza matokeo ya wajumbe na nafasi za wagombea wa viti maalumu, nafasi ya uenyekiti haitatangazwa hadi taratibu nyingine za uchaguzi zitakapoandaliwa,
alisema Hida.
Mkoani Arusha msongamano wa kupiga kura, katika kituo cha Mbauda, Kata ya Sombetini unadaiwa kusababisha kifo cha mtu aliyetambulika kwa jina la Suleiman Bakari.
Tukio hilo lilitokea saa tatu asubuhi katika kituo hicho ambacho kilikuwa kimefurika watu. Mjomba wa marehemu, Ramadhani Athumani alisema kifo hicho kimewashtua kwani marehemu hakuwa mgonjwa.
Marehemu alikuwa ni kinyozi na baada ya kupiga kura alianguka ghafla,
alisema.

0 comments:

Post a Comment