Dec 15, 2014

MWALIMU WA SEKONDARI AUAWA KWA KUCHINJWA HUKO BUKOBA,
 Kanisani alipouawa mwalimu Ng"wandu
Ni katika kipindi cha miezi miwili tu, kuanzia Octoba 9 hadi Desemba 4 mwaka huu, ambapo jumla ya vijana  6 wameuawa katika mazingira ya kutatanisha,  watatu wamechinjwa katika kata ya Kitendaguro, 1 katika kata ya Rwamishenye, huku wawili wakichinjwa katika kata ya Kibeta ndani ya manispaa, huku wananchi wakishangaa ukimya wa mamlaka bila kuchukua hatua.

Tarehe 09 Oktoba, aliyeuawa mwalimu DIONIZ NGW’ANDU wa shule ya sekondari Kagemu, alipokuwa katika kanisa la PAGT, baada ya kukatwa kichwa na kitu chenye ncha kali, huku jamaa yake aliyekuwa mlinzi katika kanisa hilo siku hiyo akijulikana kwa jina mojala THEMISTOCRES akisalia na ulemavu wa maisha, kama alivyoeleza  mchungaji wa kanisa hilo FAUSTINE JOSEPH.

Siku kati ya 5 au saba badaaye, mwili wa kijana ambaye hakutambuliwa majina wala sura, ulikutwa umeharibiwa kwa kunyofolewa macho, huku ukitupwa kando mwa shamba la mmoja wa wakazi wa Kitendaguro, ambapo Anakret Laurent Kyaishozi miaka 30 alikuwa shuuda, aliueleza mtandao huu kuwa mwilihuoulichukuliwa na polisi mpaka sasa hawajajua ninikiliendelea.

Kando na hayo, familia ya kijana aliyekuwa na umri wa miaka 37 Erick Kashaga akiacha mjane Sofia Mozes miaka 32 na watoto saba, imesalia katika mvutano mkubwa,na familia ya bwana Levocatus , ambaye mpaka sasa yuko mikononi mwa jeshi la polisi, huku jamaa zake wakielezwa kuwa uchunguzi unaendelea.

Kaburi la Mozes Kashaga
 Revocatus ni kijana  mwenye umri wa miaka 33 huku akiwa na watoto watatu wawili wakizaliwa na mke wake wa Katoma walieachana, na mmoja akizaliwa na mke anayeishi naye Kitendaguro, Bi Ajat au Betrida mwenye umri wa miaka 32, alikamatwa baada ya kutajwa kuwa alitambuliwa na kijana aliyekuwa na marehemu wakati wa tukio .
Mzee Rumumba akionesha eneo alipochinjwa Mozes
Mzee SILIDION RUMUMBA mwenye umri wa miaka 73,  ndiye mmiliki wa kilabu cha pombe, ambacho dakika za mwisho marehemu aliondoka hapo muda wa saa tano usiku, akiwa na jamaa zake wawili.

Ndani ya dk kama mbili baadaye, liyetajwa kwa jina moja tu la Eriki alirudi nyumbani kwa mzee SILIDION RUMUMBA akiwaeleza kuwa wamevamiwa na mtu ambaye alimtaja jina, huku akisema kuwa hana uhakika kama watamkuta hai Kashaga, ilhali akitoa taarifa hizo kimyakimya, pasi na kupiga kelele wakati wa tukio,jambo ambalo linawashangaza wengi, kwasababu marehemu ameuawa karibu kabisa na makaazi ya watu.
Mama mzazi wa Mozes

Kando na maelezo hayo, nimetaka kusikiliza ushuuda wa Erick aliyethibitisha kuwa alishuudia mauaji hayo, lakini nyumbani kwaojamaa zakewalisema kuwa huwezi kumwona sababau wamemficha sehemu baada ya kutishiwa na mkewa mtuhumiwa.
Hayo yamesalia katika familia hizo ndani ya kata ya Kitendaguro, huku katika kata ya kibeta, lawama kubwa zikiangushwa kwa mamlaka, kuwa hawajaonesha juhudi zozote  baada ya kuuawa kijana GOODRUCK FRANCIS aliyekuwa na umri wa miaka 38, ambapo  taarifa za awali zinaonesha kuwa aliuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana, ikiwa ni kando kando mwa barabara ya mtaa wa Kibeta Amjuju.
Bi Stella Lenatus amesema amekata tama kwasababu tangu ahojiwe, ameenda kituoni kujua taarifa za mdodgo wake na kuambiwa asubiri walikuwa bize na kazi nyingine muhimu.
 
Hapo kushoto pichani ndipo aliuawa Gudrack eneo la Kibeta Anyama.
Sambamba na wanaouawa pasipo kutambulika majina na makwao ndani ya manispaa ya Bukoba, Ernest Kato ni kijana aliyeuawa mwezi novemba akiwa na miaka32,katika mtaa wa Bugezi kata Rwamishenye, majira ya usiku, na kutambulika asubuhi ya tarehe iliofuata kwa kukutwa amechinjwa, huku akiacha mjane na mtoto mmoja, ambaye hatahivyo  amekimbia kwa kuhofia naye kuawa.

Mmoja kati ya wanafamilia wa marehemu Ernest, ameomba jina lake lihifadhiwe, pamoja na kusema kuwa wanaishi kwa hofu kubwa kiasi cha kujipangia muda wa kurudi nyumbani mapema nyakati za usiku, na shughuli zimesimama.

Mauaji ya  mwisho hadi ninakamilisha makala haya, ni alivyouawa Joran Rutulaniisa, mkaazi wa Kibeta magoti, nilifika eneo la tukio muda mfupi tu baada ya polisi kuubeba mwili wake lakini taarifa za ndugu ambao hatahivyo wanahofu ya maisha yao, ni kuwa nduguyao  ameuawa kwa aina ile ile ya vifo vya kukatwa koromeo.
 
Marehemu Rutu enzi za uhai wake
Tetesi ambazo bado sijazithibisha, wananchi wanaofanya biashara ya senene, wamelazimika kuanza kujifunga vitu vigumu na tauro shingoni, kama taadhali watakapovamiwa.
Shangazi na mama mdogo wa marehemu kwenye kaburi la Rutu

Baba wa marehemu Rutulanisa
Mauaji nikitendo kisichokubalika kwa mwenyezi Mungu, jambo linalompa shekh mkuu wa mkoa wa Kagera Aruna Kichwabuta,kukemea hali hiyo katika mamlaka na wananchi.


0 comments:

Post a Comment