Dec 6, 2014

Quick Racka Afungukia Kuwa yeye na kajala wana Uhusiano Wa Kimapenzi.

Mwanamiuziki wa kizazi kipya Quick Racka amekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na actress Kajala Masanja. Akizungumza katika XXL ya Clouds fm jana Racka aliyetoa wimbo wake mpya wa Bishoo wiki hii alisema..........


"Nasema hapana Kajala mimi sister yangu, tunafanya naye kazi na nimeunganishwa na Lamata. Lamata ni director ninayemmfahamu zamani kidogo kipindi kile tunafanya ‘Mbwa Mwitu’ tulikuwa wote, Lamatah, Hemedy! Unajua mnavyofanya movie ni tofauti na kufanya video, kwa mfano wakati tunafanya ile movie ya Wolper, tulikaa Magomeni kambini ili kujenga chemistry. Unajua mnapoigiza kuna vitu lazima viendane. Sisi ni kambi moja inabidi mchongo tuufanikishe"

alimalizia kwa kusema "I have a girlfriend, anavyosikia hivi vitu mimi kwa upande mmoja inaniharibia na sijui yeye pia ana mtu wake huko kwahiyo tuna wazazi, tuna watu wetu wa karibu ambao wanatuangalia, watu ambao wametupenda na wametuamini hivyo halafu wakija kusikia mambo haya kwenye media wataona kumbe huwa hamfanyi kazi, wao wanachukulia serious. Sio vitu vya kweli"

0 comments:

Post a Comment