Dec 17, 2014

SAD news:Aisha Madinda Afariki Dunia


Mnengueaji(dancer) maarufu wa Twanga pepeta Aisha Madinda amefariki dunia muda sio mrefu leo hii. Mkurugenzi wa band ya Twanga Pepeta Asha Baraka amedhibitisha kifo hicho.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.

Katika uhai wake Aisha alikuwa mmoja wa dancer mahiri sana na waliojizolea umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Ameen

0 comments:

Post a Comment