Jan 6, 2015

Aingiziwa chuma sehemu za siri na mume wake kutokana na wivu wa mapenzi.

Akisimulia mkasa huo akiwa hospitalini,mwanamke huyo alisema siku hiyo mumewe ambaye alikuwa amelala kwa mke mkubwa alifika nyumbani na kumkuta akiwa anakamua ng’ombe maziwa.

“Baada ya kufika nyumbani alimuuliza binti yetu niko wapi,alipoambiwa ninakamua ng’ombe alinifuata na kuanza kunigombeza kuwa usiku wa siku hiyo niliingiza mwanaume na kufanya nae tendo la ndoa,nilijitetea sijafanya hivyo lakini akaanza kunishambilia kwa kipigo na kuninyonga shigo kwa kutumia kitenge hadi nikaanguka na kupoteza fahamu”alisema mwanamke huyo.
“Nilipozinduka nikajikuta mimi na binti yetu wa miaka 13 tumefungwa mikono huku nikiwa na chuma aina ya nondo sehemu za siri,baadaye akatufungulia na kuanza kutupiga tena kabla ya kutokomea.

Ukatili wa kijinsia unaendelea kutikisa Mkoa wa Mara mwanamke huyo ajulikanae kwa jina la Rhobi Mwita amelazwa katika hospitali teule ya wilaya ya Bunda baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa kuingizwa chuma sehemu za siri na mume wake Mwita Chacha kutokana na wivu wa mapenzi.

Muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo Ester Maduhu alisema mwanamke huyo alipokelewa akiwa na hali mbaya na kwamba kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.

0 comments:

Post a Comment