Jan 25, 2015

JE UNAJUA?, MWANAMKE HAVUTIKI KIMAPENZI NA MWANAUME ANAE PENDA SANA

Mwanaume mtakatifu ni yule anaemwachia maamuzi yote mwanamke, anaona kuonyesha upendo wa hali ya juu ndo kutamfanya mwanamke akae na kupendezwa na yeye zaidi, Mwanamke anapenda mwanaume kiongozi, anayejiamini na kujua jinsi ya kujisimamia. Ninajua hili litakushangaza, Mwanamke anapenda kupewa vikwazo na kuchemshwa akili, maana kunamfanya awe anakufikiria zaidi na kukutaka kukujua na kukubadilisha hii inamfanya hamasa yake juu yako kuongezeka na kuvutiwa na wewe zaidi, iwapo akikuzoea na kukuona wa kawaida na kukukariri kila kitu unachofanya hamasa zake hupungua na kukuona kama unaboa maana kunakua hamna kitu kinachomshangaza kuhusu wewe na hapo ndipo nguvu ya mahusiano hubadilika na kumfanya yeye kuwa na sauti ndani ya mahusiano na kukuona kama hauna kiwango cha kuwa mwanaume wake.Hivi ni vitu vinavyoweza kufanya uonekane mwanaume mtakatifu na kukusababishia kupungua kwa nafasi ya kumpata mwanamke umtakaye na kama tayari unae basi wewe unakua hauna nguvu kwenye mahusiano na kumfanya mwanamke kukuendesha kama gari bovu.


1, Unamkubalia kwa kila kitu anachotaka.
Msimamo na kujiamini ni kitu ambacho ndicho hukutengenezea heshima kwa mwanamke, unatakiwa uonyeshe uanaume wako, akikwambia kitu kiangalie kwa marefu na mapana na toa jibu kulingana na uonavyo na si kukubaliana nae kwa kila kitu, hii itamuonyesha jinsi ulivyo mwanaume kiongozi na iwapo ukianzisha familia nae atakua na imani nawe kuongoza familia, iwapo ukimkubalia kwa kila kitu anachotaka atakuona si mwanaume halisi na kukudharau maana utaharibu maisha yake.

2, Unahisia kupitiliza, unamuhitaji kuliko.
Kila kitu kinanafasi, ukikizidisha hauwezi kuuona uzuri wake tena. Hata mapenzi nayo yanahitaji nafasi, ukimuhitaji mwanamke muda wote unataka kuwa nae mapenzi hayawezi kunoga zaidi, atakosa hata muda wa kukumisi na kusababisha hamasa zake kushuka sababu ya kukuzoea na kukuona wa kawaida, na hata kama ulikua ndo unamtongoza ataishia kukuchukulia kama rafiki tu.


3, Unaomba msamaha kwa kila kitu.Kila kitu si cha kuomba msamaha, ukiwa unaomba msamaha kwa kila kitu unakua unapoteza thamani ya neno na kumfanya msichana asijisikie vizuri na kukuona wa ajabu na unakua unajishushia heshima yako kwa ujumla.

4, Unaaibu kupindukia.Aibu mara nyingi inatokana na kutojiamini na kutojua thamani yako, kitu cha kwanza mwanamke anachopenda kukiona kwa mwanaume ni jinsi anavyojiamini, aibu itakufanya thamani yako ipungue kwake na hata kama alikua amependezwa na wewe basi hamasa itaanza kupungua.5, Unamsubiri kwa kila kitu mpaka aanze yeye.
Mwanaume kwa mwanamke ni kiongozi, iwapo utashindwa kuwa na msukumo wa kuanzisha mambo atakuona kama ni mtu usiejua jinsi ya kujisimamia na wala huwezi kufanya kitu chochote cha maendeleo na itasababisha akudharau kwa hilo na utapoteza sifa ya kuwa nae.

6, Hauwi mbunifu.Mapenzi yanahitaji ubunifu, na kama mwanaume unatakiwa kuwa mbunifu wa kubadilisha mambo na mazingira ili kumuongezea hamasa juu yako, jua jinsi ya kumfanya atabasamu ambapo amenuna, na kumfanya avutike zaidi na kupendezwa zaidi na wewe, usipokua mbunifu na kufanya mambo yale yale utamboa na atakuona wa kawaida na kufanya hamasa yake kupungua na ndivyo na thamani yako itakua inaisha.

7, Huonyeshi mipaka yako na hausemi hapana.
Kila mtu anamipaka yake, iwapo amekuudhi hakikisha unafanya kitu kitakachomfahamisha amevuka mipaka, kama kuna kitu kmekukera sema hapana, onyesha unavyojiamini na usionekane bwege na kukufanya akudharau, kama kitu hakiendani nawe onyesha, hii itatengeneza heshima na kufanya avutike na wewe zaidi, tofauti na hapa ukiwa ni mtu wa kucheka cheka tu lazima akudharau.

8, Unaona heri akuumize moyo kuliko kuachana nae.
Kung'ang'aniza mapenzi ni kitu kibaya sana, kunamfanya mwenza wako akudharau na kukuondoa kabisa moyoni, na hata kama kulikua na hamasa ndogo imebaki basi lazima ipotee, jua mipaka yako na kama mapenzi yamefika mwisho jua muda wa kuondoka.


9, Unatumia muda mwingi na yeye pamoja na marafiki zake.Marafiki wake wakikuzoea sana, dharau huanza maana utakua mtu wa kawaida tu, na marafiki zake wakishakudharau ujue huna nafasi tena.

10, Unamnunulia zawadi kila muda bila sababu na kutoa sifa pale zisipohitajika.
Zawadi ikizoeleka inapoteza uzito wake na sifa nazo vivyo hivyo zikiongewa sana zinakua hazina mvuto tena zaidi ya kushusha hamasa yake na kukuona wewe ni wa mzaha.

0 comments:

Post a Comment