Jan 21, 2015

JINSI YA KUONGEA WAKATI WA UTONGOZAJI,ILI UKUBALIWE KWA HARAKA


"Ulishawahi kujikuta unatamani kuliko kumtongoza msichana mzuri sehemu flani japo upate namba yake ya simu ila unajikuta huna jinsi yeyote au wazo juu ya nini cha kufanya au kuongea, unatamani kumfata nguvu miguuni zinakua zimekuishia unashindwa hata kupiga hatua moja kumsogelea, lile wazo pekee la kutaka kumsogelea linakufanya moyo uwende mbio, mikono iloane na jasho jembamba kukutoka huku akili yako ikishindwa kufikiria vizuri nini cha kuweza kuongea iwapo ukimsogelea?."

Unajua nini?, 

Kujiamini ni kitu kinachochukua nafasi kubwa na ndo msingi mkubwa katika mahusiano na hasa wakati wa utongozaji, na ndicho kitu mwanamke hutumia kumpima mwanaume na kumpa nafasi ya uwezekano wa kuwa na yeye au la, ila mara nyingi mtu hushindwa kujiamini kutokana na hofu ya kutokujua ni nini cha kufanya au kuongea wakati wa utongozaji.


Mwanamme ambaye huwa hafanikiwi kwenye utongozaji hufanya makosa madogo madogo kama kumpandisha hadhi mwanamke anayemtongoza mpaka kiasi ambacho anaifanya hadhi yake binafsi kuonekana ndogo na siyo tu anamtongoza mwanamke kwa wasiwasi na kutojiamini, bali anamtongoza  ovyo  bila mpangilio na zaidi ya hapo anamuweka wazi mwanamke kwamba anataka kumjua zaidi ya kawaida na anahitaji  huyo mwanamke apendezwe naye hapo hapo.


,Mtaalamu wa utongozaji huwa anasubira na huwa hapaparuki, kutongoza ni sanaa na inahitaji uwelewa mkubwa na hata mimi iwapo ningelikua ndo huyo mwanamke sidhani kama ningelikubali hivi hivi, lazima atake kukujua kwanza ndo mambo mengine yafuate.Nayajua haya kwa sababu kwa muda mrefu na mimi nilikua na paparuka ovyo.


Ukitaka kuishia kusonywa na matusi juu ingia na mstari wa "Dada samahani nimetokea kukupenda nataka tuwe wote, kila nikikaa nakuwaza wewe, nikinywa maji nakuona kwenye glasi",
 bila kuangalia mazingira na papara za kusema yaliyo moyoni mwako, huu mstari lazima utakutokea puani, mwanadada ndo amekuona siku hiyo hiyo, hata alikua hajui mtu kama wewe upo katika hii dunia, hakujui na unategemea akuambie anakupenda pia, we vipi?, hapo unapoteza nafasi na utaishia kuambiwa usiyoyataka na kuumia moyo tu.


Naamini kabisa mwanaume yeyote mwenye mtazamo sahihi na mwenye hamu ya kujifunza anaweza kuelewa jinsi ya kutongoza mwanamke sehemu yeyote na mahali popote pale, kutongoza hakuitaji kukalili mistari ya kutongozea wala kumpulizia dawa kutoka kwa mganga,


Mwanaume mtongozaji hajishushi na anatumia mbinu ya kuonyesha ujasiri wa kimaongezi na akiongea na mwanamke, mwanamke hutambua ya kuwa huyu jamaa ana nia naye kutokana na lugha anayoitumia wakati wa maongezi.


Makosa makubwa mawili ambayo nilikua nafanya wakati wa kutaka kumtongoza msichana, nilikua nasubiri na kusita kwa muda mrefu na kutojua nini cha kuzungumza.


"Unakuwa na dakika tatu kutoka unapomuona msichana anayekupendeza na mpaka pale utakapomsogelea na kuanzisha mazungumzo yanayompendeza, ukisubili sana nafasi yako itakupita kama upepo na kupoteza nafasi hiyo muhimu".


Kama ni kwenye sherehe ndipo ulipomuona, piga moyo konde na mwendee na mwambie,
>>"Nimekuona kutoka mbali ila moyo wangu ukang'ang'ania mpaka nije nikusalimie, mambo?"
>>"Siku yako inaendaje?"
>>"Upo upande wa bibi harusi au bwana harusi?"
>>"Oooh, upande wa bibi harusi, ndo maana dada yako amewahi kuolewa!, ukoo wenu mzima inavyoonyesha umelaaniwa kwa uzuri!"


Mchokoze kwa maneno matamu, muulize maswali ya kumfanya afurahie maongezi na kama ukiwa unatoa sifa ifiche ndani ya sentensi inayovutia, ukitaka kumjua uliza maswali ambayo majibu yake ni mepesi na rahisi, kama ukitaka kujua anachofanya muulize,


>>"Kwa hiyo familia nzima mwanafunzi amebaki ni wewe tu, maana dada yako tayari ameshaolewa?"

Kwa maswali ya namna hio atajikuta anajiongelea kuhusu yeye na kukufanya akuzoee mapema, na ukiona maongezi yanaelekea ukingoni unatakiwa unakuwa shapu na mbunifu kwa kuanzisha mada nyingine inayovutia zaidi, itakayoleta maongezi matamu zaidi.

Kujua kitu cha kusema wakati wa kutongoza ni ngumu, ila inabidi ujiamini na ufanye kujisahau na kuweka akili kama upo unaongea na dada yako ila maongezi yaweke yawe ya kuvutia zaidi na uyapambe kwa sifa bila kuonyesha nia yako moja kwa moja, mwisho wa maongezi muombe namba ya simu au omba umtoe mtoko akuonyeshe maeneo hayo maana wewe ni mgeni na maongezi yamekupendezea na ungependa kuyaendeleza siku nyingine.


"Ukweli ni kwamba haijalishi utakachokiongea, unaweza ongelea kitu chochote kile ili mradi maneno yawe katika hali nzuri kihisia, onyesha tabia ya kujiamini na mipaka yako."


Acha kuwa na wasiwasi na kufikiria nini cha kuongea, we mfate kwanza na maongezi yatajitengeneza yenyewe kwa jinsi ya mazingira mliyopo na weka akilini kitu kimoja, huyo msichana unayeenda kumtongoza inawezekana anatongozwa mara tano au zaidi kwa siku tokea alipokuwa na miaka kumi na nane, kwa hiyo inawezekana ameshatongozwa zaidi ya mara 1000, kwa hiyo usifanye vitu ambavyo ameshavizoea kila siku na kuishia kutoa maamuzi ya kutokubali maombi yako kama wengine waliokataliwa waliotoa maombi yao hapo mwanzo kabla yako, kuwa mbunifu na tumia mazingira yako kwa usahihi na uzuri zaidi.


Hakikisha katika maongezi yako usigusie vitu vifuatavyo,
kUsimsifie sana, atakuona kama unambeza.Usijaribu wala kumuuliza kama ana mtu, ana mshikaji wake au anamahusiano na mtu yeyote yule.Usimuulize maswali magumu ambayo yanahitaji uelewa wa kitu fulani.

Vitu vifuatavyo ni ambavyo hutakiwi kuvifanya wakati wa utongozaji,

 • Usiongee kwa sauti ya juu sana,
 • Usijibu kitu au jambo kwa haraka sana,
 • Usiwe unaondoka ondoka au kuhamisha mapozi, usiwe na papara na kuwa mtulivu.
 • Kitu cha kuweka akilini zaidi usifikilie sana unachokiongelea, ukifikiria sana utakaribisha wasi wasi na kutokujiamini.

Wakati wa maongezi yako ya utongozaji, hakikisha unahusisha mambo yafuatayo,

 • Vitu ambavyo anashauku navyo na anavipendelea,
 • Vitu ambavyo unashauku navyo,
 • Hadithi zenye vichekesho na mguso wa mahaba,
 • Jifunze jinsi ya kuhadithia hadithi za kuvutia,
 • Mfanye acheke na kutabasamu kwa kile unachokiona,
 • Michezo ya furaha na ya kuvutia,
 • Unaweza kujikweza kidogo ila usipitilize.
Endelea kufuatilia blog hii mpaka hapo  tutakapo kuletea mada nyingine tena.Asanteni wote wasomaj wetu.

0 comments:

Post a Comment