Jan 27, 2015

MAMA AUA WATOTO WAKE WAWILI KISHA KUWAZIKA NDANI YA NYUMBA YAKE HUKO TABORA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili mmoja wa miaka minne, na mdogo wake wa miezi minne wameuawa na mama yao , Zuhura Steven, aliyedhaniwa kutokuwa na akili timamu, na kufukiwa katika mashimo mawili tofauti, katika nyumba walimokuwa wakiishi, huko katika mtaa wa Salimini kata ya Chemchemu manispaa ya Tabora.


Wakizungumzia tukio hilo linalodhaniwa kutokea kuanzia asubuhi ya terehe 25/01/2015, hadi walipogundua tukio hilo usiku  saa moja.
Mwenyekiti wa mtaa wa Barehani pamoja na wananchi walioshuhudia tukio hilo usiku , wanasema mchana kuwa watoto hao hawakuonekana kama mazoea yao wakicheza.
Aidha kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Juma Bwire, pamoja na matukio kadhaa yaliyotokea, akizungumzia tukio hilo amewataja marehemu kwa majina ya Mwamvua Mrisho (4) na Soud, ( miezi 4) jeshi la polisi linasikitishwa tukio hilo  la kikatili, ambapo amesema upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Via>>Itv

0 comments:

Post a Comment