Jan 28, 2015

NAMNA YA KURUDIANA NA MPENZI WAKO ULIEKOSANA NAE NA BADO UNAMPENDA

Hivi karibuni msichana wako ameamua kuachana na wewe au labda wewe ndie uliyeamua kumuacha ila baada ya maamuzi hayo kupita na kufanyika, moyoni unahisi upendo wako juu yake bado umeutawala moyo wako na bado anaumiliki tena kwa sehemu kubwa sana na hauko tayari kumwachia aende kwa kuwa umeshaona wazi ya kuwa maamuzi uliyoyafanya au yaliofanyika yana makosa makubwa.

Njia itakayokusaidia kurudisha muda nyuma na kuwa naye tena, kukurudishia yule mmoja umpendae ambaye juu yake ndio moyo wako unapokamilika, njia hii itategemeana sana na hali ya mwenza wako mlieachana na jinsi anavyojisikia juu yako kwa kile ulichotenda au kumtendea.

1. Yatambue makosa.

Unaweza fikiria unachofikiria kichwani mwako ila lazima huyo msichana atataka kujua ni nini kilichosababisha wewe kubadilika, wanawake wa karne ya digitali huitaji majibu ya sababu sababishi ya kile kilichokusababisha ubadilike kiasi cha huo uwamuzi kufanyika, uwe umesababisha wewe au yeye majibu yanatakiwa, na mwelezee kwa umakini utafanya nini ili kuibadilisha hio hali na kumpa mikakati thabidi na kumuonyesha nia ya kuyatatua hayo matatizo.


2; Omba msamaha na onyesha hisia ya kuwa unamaanisha.

Wanaume wengine hujiona ngangali na kuona hali ya kuomba msamaha ni kujishusha, na inawezekana kabisa alishawahi kukutana na hio hali kwenye uhusiano uliopita, muonyeshe una nia ya kubadilika badala ya kujielezea na kuomba msamaha, muonyeshe nia yako kwa matendo, kama ulikuwa unachelewa kupokea simu zake badilika wewe ndo uwe wa kwanza kumtafuta.

3; Mpe muda.

Mpe muda wa kufanya maamuzi yake, maamuzi makubwa kama hayo huwa yanachukua muda kuamuliwa, usiwe na haraka ya kutegemea majibu hapo hapo, kama kweli unamuhitaji mpe muda wa kufanya maamuzi yake mwenyewe iwapo anataka kuwa na wewe au la, inaweza kumchukua sikua au hata wiki mpaka aweze kukuamini tena na kukukabidhi moyo wake, kuwa mvumilivu na usikurupuke na kulazimisha mambo kwani itakuweka mahali pabaya zaidi ya ulipokuwa

0 comments:

Post a Comment