Jan 28, 2015

Ommy Dimpoz, Idris wawaliza walimu waoMSANII nyota wa Bongo Fleva Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz,’ na mshindi wa shindano la Big Brother Afrika 2014, Idris Sultan, wakisalimiana na walimu wao.MSANII nyota wa Bongo Fleva Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz,’ na mshindi wa shindano la Big Brother Afrika 2014, Idris Sultan, juzikati waliwaliza machozi ya furaha walimu wao wa shule ya Mbezi High School iliyopo Kimara walikosoma, baada ya kufika ghafla kwa ajili ya kuwasalimia.
Dimpoz alimaliza kidato cha nne mwaka 2009 wakati Sultan alifanya hivyo mwaka juzi na ujio wao ulileta bashasha kubwa kwa walimu na wanafunzi waliowalaki kwa furaha na kupiga nao picha pamoja na kumtaka mkali huyo wa kibao cha Me and You kuwaimbia kidogo, kitu ambachoalikifanya.


Wakiongea na wanafunzi wa shule hiyo

“Tuliamua kwenda shuleni baada ya kugundua kuwa wote tulisoma pale, nilikutana na walimu walionifundisha pamoja na baadhi ya wafanyakazi, hii ilitufariji sana. Tumekubaliana kwamba wakati wa mahafali yao tutakuwa tukifika ili kuwapa sapoti kama wakati huo tutakuwa tupo hapa mjini,” alisema Dimpoz, ambaye anafanya vizuri katika muziki huo wa kizazi kipya.


Source: GPL

0 comments:

Post a Comment