Jan 31, 2015

Picha: Zari ndani ya Dar, athibitisha kwa mara ya kwanza kwa kauli yake kuwa mpenzi wa Diamond


Katika mitoko yako ya weekend hii usije kushtuka utakapokutana na couple fulani ‘Ameizing’ ya TZ+UG, sababu Zari Tlale a.k.a The Boss Lady yupo ndani ya jiji la Dar au kama anavyopaita mrembo huyo D-City.

Kupitia Instagram mrembo huyo wa Uganda ambaye makazi yake yako Afrika Kusini amepost picha kadhaa akiwa na mpenzi wake Diamond Platnumz kwenye gari ya staa huyo aina ya BMW.Katika picha nyingine inayothibitisha uwepo wake ndani ya jiji la joto, ni picha aliyopiga na mpenzi wa dancer wa Diamond, dumyutamu anayejiita jujudumyz.

Kwenye moja ya picha hizo ameandika : “Another beautiful day in D-City”, na kwenye picha nyingine ameandika moja ya misemo inayovuma kwa sasa hapa mjini “Kishkwambiii”.Licha ya kwamba Diamond na Zari kwa sasa wanajulikana kuwa ni wapenzi, lakini mara zote walipoulizwa juu ya uhusiano wao wamekuwa wakikanusha na kusisitiza kuwa wana project ya pamoja. Lakini safari hii Zari amethibitisha mwenye kwa kauli yake baada ya kumuita girlfriend wa dancer wa Diamond “wifi”.Kwenye picha aliyopiga na msichana huyo Zari ameandika: “With wifi @jujudumyz out and about

Hivi karibuni Diamond alithibitisha kuwa anategemea kupata mtoto na Zari baada ya kupost picha ya Ultra Sound ikithibitisha kuwa Zari ni mjamzito. Hivyo huenda Diamond atakuwa anafurahia kukishika kitumbo kinachokua cha Zari ambamo ndani yupo Chibu Junior.

0 comments:

Post a Comment