Jan 4, 2015

WATOA MWILI WA MAREHEMU KABURINI NA KUUPASUA

kumetokea vurugu za aina yake katika makaburi ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga wakati wa mazishi ya mwanamke mmoja aitwaye Benadetha Steven(35) aliyekuwa anaishi katika mtaa wa Mapinduzi maarufu mtaa wa Juma Matv katika kata ya Ndala aliyefariki dunia juzi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.


Tukio hili limetokea  wakati wa mazishi ya mwanamke huyo anayedaiwa kufariki dunia kutokana na uvimbe wa tumboni uliokuwa unamsumbua hivyo ndugu wa marehemu kuamua kumfanyia mambo ya kimila.

Habari zinasema kuwa ndugu wa mwanamke huyo anayetokea Musoma (Mkurya) walikuwa wanataka ndugu yao apasuliwe tumbo wafanye mambo ya kimila makaburini ili kuondoa mkosi katika ukoo  lakini uongozi wa eneo husika wakasema utaratibu huo ni vyema ungefanyika hospitalini badala ya hadharani watu wakishuhudia.

“Mgogoro ulianzia nyumbani hata  kabla ya kwenda makaburini,ndugu walionekana kuelewa wakatulia na wakati mazishi yanaendelea ndipo ndugu mmoja wa marehemu akaingia kaburini,akiwa amevaa mipira ya mkononi,akiwa na wembe na boksi dogo lililokuwa na kifaranga cha kuku na kuzuia waombolezaji wasitupie udongo kaburini”,alieleza mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Sijali Jumanne 


"Ndugu huyo wa marehemu aliingia kaburini baada ya mchungaji kumaliza ibada ya mazishi na kuruhusu mwili wa marehemu ufukiwe,ndipo akaanza kuuchana kwa wembe,akachinja kuku,kisha kumwagia damu marehemu na kumwingiza kuku huyo kwenye tumbo la marehemu,akafunika jeneza na ndugu wakaendelea na mazishi”,aliongeza Jumanne.

Shuhuda huyo alisema kitendo cha ndugu wa marehemu kung'ang'ania kufanya mambo yao ya kimila tena hadharani,kiliwakera wananchi wakaamua kutoka makaburini,na jeshi la polisi likafika eneo la tukio na kuwakamata ndugu wote wa marehemu.


Mwenyekiti wa mtaa wa Mapinduzi  Ayubu Daniel alikiri kuwepo kwa tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment