Feb 3, 2015

JINSI YA KUMPATA UNAYEMTAKA KIMAPENZIKuna wanaume wengi wamekuwa wakikosea kutongoza.Wapo wengine labda amempenda binti fulani lakini anashindwa cha kufanya.
Kuna wakati unaweza kukuta mwanaume anachokifanya anampa ofa mwanamke,mara anamwambia tukale na hata zawadi nyingine zinafuata.
Jambo lililo la msingi katika maisha yetu ni kuwa wazi,mtu aelewe nini hasa unachokitaka moyoni mwako si zaidi.


Wapo ambao wanaogopa watu labda ni kwa sababu ni wazuri au wamesoma zaidi yao,lakini mapenzi ni zaidi ya hayo,unaweza kuona mtu kweli anaonekana yuko matawi ya juu jina tu,mapenzi hayana matawi ya juu wala ya chini
Ndo maana unaweza kuona mama mtu mzima na heshima zake anajisalimisha kwa kijana mdogo,au unaweza kuona mwanaume mtu mzima na hekima zake anafanya ngona na mfanyakazi wa ndani,huenda akawa mchafu au hata si wa kutamanisha kivile.


Mapenzi ni suala pana,unaweza kujiremba ukifikiri ndo njia ya kumtamanisha mwanaume,wapo wanaume wanachokipenda sio mwanamke ajirembe.

Unaweza kuvaa kimini na nguo yenye kuonyesha sehemu kubwa ya mwili wazi,wapo wanaume wenye kuchukia hilo.

Unaweza kuvaa suruali ukifikiri ndio chaguo la wanaume,wapo ambao hawataki kusikia mwanamke anayevaa suruali.Ninachotaka kusema ni kwamba watu wametofautiana kwa namna ya mahitaji yao.HATUA MUHIMU UNAPOFIKIRIA KUTONGOZA:

Jambo la kwanza lililo la msingi ni kufahamu anachokipeanda yule unayetaka kuanza kumfuatilia.Je ni mwenye kupenda hali gani,yuko makini au hayuko makini. Furaha ya wanawake wengi ni kuwa na mwanaume ambaye anajiamini.

HATUA ZINGINE:

  1.  Mguse bega au sehemu ambayo si ya kumdhalilisha,mwambie du umependeza;kama uko kwenye mazingira ambayo yanawezekana,Inashauriwa kumgusa kama unataka kuuliza jambo fulani,Hili ni jambo la msingi kwani kitaalamu linachangia kumjua mtu tabia yake na anavyoweza kukuchukulia katika mambo mengine unayotaka kuyasema.
  2.  Wanaume wengi wanakosea kwa kuomba namba za simu,lakini kitaalamu njia inayokubalika ni wewe mwanaume kumpa namba yako huyo mwanamke ambaye unafikiria kuanzisha mawasiliano nae kwa lengo kwamba mwisho wa siku awe mkeo.Au wakati mwingine unaweza kumpa simu yako ili aandike namba yake.
  3. Kama mnaweza kupata muda,mkaribishe sehemu kwa ajili ya kuongea zaidi.Mara nyingi usianzishe mazungumzo ya kumwambia mtu nataka kuoa,hata kabla hamjakaa na kusomana hata kama kwa sekunde kadhaa.Ni aibu kuambiwa sikutaki au nina mwingine,lakini ukianza kwa vitendo,unaweza kujua kama hapa kuna dalili au kuachana na kile unachotaka kukisema.
Hata katika maisha ni vizuri kuwa mwangalifu kabla ya kuamua kumtongoza fulani na kukubaliana na fulani,pata muda wa kumchunguza kwani safari ya ndoa ni ndefu,inahitaji kuwa na mtu ambaye kweli atakufaa.

0 comments:

Post a Comment