Mar 16, 2015

JE WEWE NI MBAYA? JUA DALILI ZA MDADA MWENYE SHEPU NA SURA MBAYA

Blog yenu imechukua muda wa miezi miwili kufanya utafiti huu ambao utawasidia sana wadada ili wengine wapunguze muda wa kujiangalia kwenye kioo na kufanya shughuli nyingine, pia kuwapunguzia muda wa kwenda saluni na kupoteza pesa ambazo wangeweza kulipia kodi ya nyumba zao. Blog yenu imeweza kupata utafiti utakaoweza kukusaidia mdada ujijue kama wewe ni mbaya au mzuri. Kama we mbaya kwanini uhangaike tena sijui, saluni, kujinyima msosi ili uwe slim, kuhangaika kununua kioo, yote haya utakuwa huna haja nayo na fedha unayoipata ukaitumia kwa shughuli za maendeleo kama vile kufuga kuku au kilimo cha kufa na kupona. Sasa utajijuaje kama wewe ni mbaya?

1. Ukiona umejipiga ‘selfie’ au hata picha yoyote ukaiweka kwenye facebook na kutag watu mia ukapata ‘likes’ mbili tu ni dalili ya wazi kuwa we mbayaaa.

2. Ukiona wakaka wanapenda sana kampani yako lakini kila mara wanakuuliza ushauri juu ya kuwapata wadada wengine , ujue wewe ni mbaya, maana wanajiona kama vile wanaongea na mwanaume mwenzao

3. Ukiwa na wasichana wenzio halafu mnataka kupiga picha ya pamoja ukona wanang’ang’ania wewe ndio uwapige picha ni dalili ya wazi hawataki uwaharibie picha yao kwa sura yako mbaya.

4. Jina lako instagram na facebook pia ni dalili tosha kuwa na wewe unajijua ni mbaya, majina kama sexydiva, sweetylicious, cutebaby na kadhalika, ni nja ya kisaikolojia ya wabaya kutaka kuonekana wazuri.

5. Ukiona utafiti huu umekuudhi na una ulaani hiyo ndio dalili ya ukweli kuwa wewe mbayaaaaa

0 comments:

Post a Comment