Mar 23, 2015

Video: Mcheza Mieleka wa Mexico afia ulingoni mbele ya maelfu ya watazamaji na Rey Mysterio anaweza kushtakiwa kufuatia kifo cha mchezaji huyoMcheza Mieleka maarufu wa Mexico Hijo del Perro Aguayo, amefariki dunia akiwa ulingoni mbele ya maelfu ya watazamaji weekend iliyopita.Mwana mieleka huyo alikuwa akipambana na Rey Mysterio Ijumaa iliyopita. Alikimbizwa hospitali lakini madaktari walithibitisha kuwa amefariki dunia saa saba usiku March 22.


Hijo del Perro Aguayo (35) ni mtoto wa mchezaji mkongwe wa mchezo huo wa Mexico Pedro ‘Perro’ Aguayo.


Uchunguzi kuhusiana na uwezekano wa kosa la kuua bila kukusudia, umefunguliwa baada ya mtoto wa mcheza mieleka maarufu wa Mexico kupoteza maisha baada ya kupigwa wakati wa mechi.


Pedro Aguayo Ramirez aliyejulikana kwa jina la Hijo del Perro Aguayo alifariki baada ya kupigwa teke na Rey Mysterio


Taarifa kuhusu kuanza kwa uchunguzi huo imetolewa na ofisi ya mashtaka ya jimbo Baja California.

Pedro Aguayo Ramirez, aliyejulikana kwa jina la Hijo del Perro Aguayo, alianguka na kupoteza fahamu kwenye kamba za ulingoni baada ya kupigwa teke na mchezaji mieleka wa zamani wa WWE, Oscar Gutierrez, maarufu kama Rey Mysterio Jr. kwa mujibu wa video ya mechi hiyo.


Rey Mystereo

Pambano hilo liliendelea kwa karibu dakika mbili kabla ya kugundua kuwa Aguayo alikuwa ameumizwa vibaya.

Alipelekwa kwenye hospitali lakini alifariki baadaye, jana Jumapili.

Aguayo, 35, alipigana mieleka kwa miaka 20 na alikuwa mtoto wa Pedro “Perro” Aguayo, ambaye kwa sasa amestaafu.Aliwahi kushinda mataji mengi ikiwemo ushindi wa uzito wa juu wa taifa na mengine. Mcheza mieleka huyo alifariki kutokana na kuumia shigo na mgongo.

Baada ya tukio hilo, Rey Mystereo alitumia Instagram kusikitishwa kwake kwa kuandika:
“I had the privilege to share a ring for the first time with Hijo del Perro Aguayo in his debut as a professional wrestler and an honor to be in the ring with this great legend for the last time! You will be missed, Perro. Just formed a friendship between brothers who opened years ago and we should not question the designs of God. But in this occasion I wonder why and I do not understand it … I take you with me for the rest of my life, rest in peace HijoDelPerro.”

0 comments:

Post a Comment