Apr 11, 2015

ACHINJA MTOTO WAKE KAMA KUKU,"ADAI KAOTESHWA NA MUNGU"


Mchungaji akiwa chini ya ulinzi.
 DUNIA ina mambo! Mchungaji wa kanisa moja mjini Harare nchini Zimbabwe, ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, amekamatwa na polisi baada ya kukutwa akitaka kumuua mwanaye wa kumzaa kwa kumchinja na kisu shingoni, kitendo alichokifanya nyumbani kwake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mchungaji huyo ambaye hata hivyo hakueleweka ni wa kanisa gani, akiwa amevaa nguo zake za kichungaji, kanzu nyeupe yenye msalaba kifuani, alimchukua mwanaye huyo wa kiume na kuanza kumchinja ndani ya nyumba yake, kabla ya kijana huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kumi, kupiga kelele za kuomba msaada.

Kwa mujibu wa mitandao, baada ya majirani kuingia ndani ya nyumba hiyo, walimkuta mchungaji huyo akiwa na kisu mkononi, ameloa damu huku kijana wake akiwa ameanguka chini akiugulia kwa maumivu makali.

Baada ya kuhojiwa sababu za kutaka kutoa roho ya mwanaye, mchungaji huyo alitoa majibu ya kushangaza;

“Nilioteshwa na Mungu, Mkuu wa majeshi. Alinitaka kumtoa sadaka mtoto wangu kama kweli nilikuwa na imani naye, sasa kwa sababu kila siku hufanya mambo yangu kwa kusikia sauti yake, nikaifuatisha. Ni kama Ibrahim alivyofanya katika Biblia.”

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kijana huyo alikuwa bado hajafariki na aliwahishwa hospitalini ambako anaendelea na matibabu wakati mchungaji huyo ameendelea kuwa mikononi mwa polisi ambao wanamhoji kabla ya kufikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

0 comments:

Post a Comment