Apr 8, 2015

BAADA YA RAIS KUSHINDA KWENYE UCHAGUZI,SASA MAKAHABA KUTOA HUDUMA YA NGONO BURE NCHI NZIMA!

Waswahili wanasema ahadi ni deni.. akina dada ambao wanafanya biashara ya kuuza miili yao Nigeria nao wanaahidi kutimiza ahadi yao ya kutoa huduma bure kwa wateja wao nchi nzima.
Chama cha wasichana hao ambao wanafanya biashara hiyo Nigeria waliahidi kwamba wako tayari kutoa huduma bure kwa mtu yoyote iwapo Rais Buhari atashinda Uchaguzi huo..

Kwa kuwa tayari Buhari kashinda wamesema watatoa huduma hiyo kwa siku tatu bure iwapo Rais huyo ataruhusu biashara hiyo kuwa halali kabisa kama ilivyo biashara nyingine.

Chama hicho ambacho kinaitwa NANP kimesema iwapo biashara hiyo ikihalalishwa itasaidia waweze kufanya biashara yao kwenye mazingira ya usalama zaidi hata Kwa afya zao.. NANP walikuwa na imani kwamba Rais Buhari ataruhusu biashara hiyo japo mpaka sasa hajatoa taarifa yoyote.

Iliwahi kusikika pia kutoka Kenya ambapo wanawake wanaofanya biashara hiyo waliandamana mpaka kwa Mwanasheria Mkuu kutaka biashara yao ihalalishwe, watambulike na walipe kodi kama wafanyabiashara wengine tu.

0 comments:

Post a Comment