Apr 3, 2015

PICHA NA VIDEO YA DAKTARI AKIBAKA WAGONJWA HOSPITALINI YAVUJA


Hili tukio huenda likakushtua kutokana na mazingira ambapo limetokea, sawa tunaenda Hospitali kutibiwa lakini wale wanaotoa huduma wakati mwingine wanakuwa na mambo yao tofauti.
Hii story unaambiwa imetokea Uingereza, Andrew Hutchinson ni nesi wa kitengo cha dharura Hospitali ya John Radcliffe Uingereza, amekutwa na hatia ya kuwabaka wagonjwa watatu walioenda kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo.

 John-Radcliffe-Hospital


Hospitali ya John Radcliffe
Muuguzi huyo anadaiwa kuwabaka wagonjwa hao waliofikishwa  kwenye Hospitali hiyo wakiwa wamepoteza fahamu, halafu akakutwa na picha na video alizojirekodi wakati akifanya kitendo hicho.

Polisi walipomkamata walikagua simu yake, computer na camera na kukuta picha hizo..

Mtuhumiwa anashikiliwa na bado uchunguzi unaendelea kwani jamaa imeonekana ana kesi pia ya kubaka watoto wawili.
Wanawake waliofanyiwa vitendo hivyo hawakujua chochote kwa kuwa jamaa aliwaingilia wakiwa hawana fahamu.

0 comments:

Post a Comment